Saturday, February 5, 2011

Thamani ya Euro kuimarishwa kwa kila hali.

Thamani ya Euro kuimarishwa kwa kila hali. Brussels, Ubelgiji 05/02/2011. Mkutano wa viongozi wa jumiya ya Ulaya umeamua kuahakikisha thamani ya pesa ya Uero in tengemaa.

Kanselah wa Ujerumani Angela Markel alisema " kwa kushirikiana na nchi wanachama wa jumuia ya Ulaya Ujerumani na Ufaransa tutailinda Uero siyo kipesa tubali pia kiuchumi na kisiasa na kuifanya iwe madhubuti katika mashindano na kuinua uchumi kwa pamoja."
Uamuzi wa viongozi wa jumuia ya Ulaya kuilinda sarafu ya Euro, kumekuja baada ya myumbo wa kiuchumi wa nchi wanachama.
Waandamanaji nchini Misri bado kushikiria msimamo wao.
Kairo, Misri -05/02/2011. Waandamanaji nchini Misri bado wanashikiria haja yao kutaka rais sasa kutoka madarakani.
Wakiongoea kupinga ombi la mkuu wa jeshi la kuwataka warudi majumbani, waandamanaji walisema "hatuwezi kuondoka hapa tulipo mpaka rais Hosni Mubaraka ametoka madarakani."
Hata hivyo jumuia ya kimataifa bado inasugua vichwa ni kwa jinsi gani wataweza kusaidia kutatua mgogoro wa kisiasa uliopo nchini Misri kwa kuzingztia nchi yenyewe ni kiungo muhimu katika eneo zima la mashariki ya kati.
Wakati maandamano ya kumpinga rais Mubara yanaendelea, bombo la kupisha gasi kuelekea nchi Jordani lilipasuka na kunamadai ya kuwa bomba hilo limelipuliwa na watu wasio julikana.
Bomba hilo lililopo Ghuba ya Sinai liliupasuka na kusababisha wimbi kubwa la moto kuelekea hewani na kuathiri usambazaji wa gasi kuelekea nchini Jordani,
Picha hapo juu ni picha ya poto ulio lipuka mara baada ya bomba la gasi kuasuka na kuathiri usambazaji wa zao la gasi kuelekea nchini Jornan.
Pichaya pili hapo juu inaonyesha waandamanaji waliopo katikati ya jiji la Kairo kwenye viwanja vya Tahrir kwa siku ya kumi na mbili tangu kuanza maadamano ya kutaka rais Mubaraka aachie madaraka.

No comments: