Wednesday, February 9, 2011

Wakili wa Charles Taylor aondoka mahakamani.

Wakili wa Charles Taylor aondoka mahamani.

Hague, Uhollanzi - 09/02/2011. Mwanasheria anaye mtetea aliyekuwa rais wa Liberia Charles Taylor ametoka mahakamani baada ya ya majiji wanaosikiliza kesi hiyo kukataa ripoti iliyo wakilishwa wakati wa mwisho.
Mwanasheria huyo kutoka Uingereza alisema " Ikiwa mahakama na sisi hatuelewani, inakuwa vigumu kuamini na wamezuia kwa asilimia 90 utetezi wa mteja wangu?"
Charles Taylor anatuhumiwa kwa makosa ya kukiuka haki zabinadamu kwa wanachi wa Sierra Leone.
Waziri mkuu wa Itali kuenda akasimama kizimbani.
Milan, Itali- 09/02/2011. Waziri mkuu wa Itali huenda akajikuta amesimama kizimbani baada ya wanasheria kufungua kesi dhidi yake kwa madai ya kutumia cheo chake vibaya.
Silvio Berlusconi, ambaye ni waziri mkuu anatuhumiwa kwa kwa kufanya mapenzi na msichana ambaye hajafika miaka kumi nane.
Mahakama jijini Milan, imeombwa ifungungue kesi baada ya kukamilika kwa uchunguzi wa kashfa hio.
Hata hivyo waziri mkuu Silvio Berlusconi amekuwa akikanisha kashfa hizo zidi yake na kusema " ni za kisiasa, wapinzani wake ndiyo wanao shikilia madai hayo ili kumchafulia jina lake."
Kampuni ya magari ya Toyota yapata hafueni.
Washington, Marekani -09/02/2011. Kampuni ya magari ya Toyota imepata hafueani baada ya ripopti ya uchunguzi kuonyesha yakuwa matizo yaliyokuwemo kwenya magari yake hayakusababishwa na mtiririko wa umeme kwenye gari.
Akiwakilisha ripoti ya uchunguzi iliyo fanywa na wanasayansi wa NASA, waziri wa mawasiliano Ray LaHood alisema "matatizo ya kuongezeka kasi ya gari wakati waundeshaji hayakusabaishwa na mtiririko wa umeme bali matatizo ya kiufundi - makeni."Baada ya ripo ti hiyo kutolewa uongozi wa kampuni ya magari ya Toyota, ulisema tutajitahidi kuimarisha magari yetu na tupo tayari kusilikiza mawazo ya wateja wetu ili kuhakikisha usalama wa kila mteja wetu.''
Kampuni ya magari ya Toyota ilipata msukosuko hivi karibuni baada ya baadhi ya wateja wake kudai yakuwa magari take yana matatizo.

No comments: