Tuesday, February 22, 2011

Muhammar Gaddafi asema hatoki madarakani

Muhammar Gaddafi asema hatoki madarakani. Tripol, Libya - 22/02/2011. Rais wa Libya melihutubia taifa la Libya na kusema hataondoka nchi na yupo tayari kufa kwa ajili ya nchi yake.

Kanal Muhammaar Gaddafi alisema, " mimi ni shujaa na mpiganaji kutoka kwenya turubai, nipo tayari kufa na nitapigana hadi mwisho, mimi siyo rais uacha madaraka, mimi ni mpiganaji."
Akiongea kwa hasira aliongezea " wale wote wananifata naawagiza wawakamate watu wote wanlioleta machafuko na wafikishwe kwenyw sheria."
"Nitahakikisha tunasafisha kila nyumba kama wasipo jisalimisha."
"Kama Libya ita yumba itakuwa makao ya Al-Qaeda."
Maandamano siyo kuaribu na siyo waasi wa nchi.
Rais wa Libya aliyasema hayo baada ya Walibya kuandamana kumtaka aachie madaraka na kuruhusu mabadiliko ya kisiasa.
Manoari za Kiiran zapita Suez Kanal kwa mara ya kwanza.
Suez Kanal, Misri - 22/02/2011. Manoari mbili za kijeshi za Iran zimepita kwa mara ya kwanza kwenye mfereji wa Suezi Kanal. Meli hizo zimepita muda wa saa tisa na dakika arobaini na tano kwenye mfereji huo na zinategemewa kurudi mwezi Tatu mwaka 2011.
Meli za Iran zimepita kwenye mfereji huo kwa mara ya kwanza tangu kuanguka kwa serikali ya Hosni Mubaraka.
Kufuatia kupita kwa meli hizo serikali ya serikali ya Izrael imesema " tunatizama kwa uangalifu mwenendo huo wa Iran."
Uongozi wa Suez Kanal uliripoti ya kuwa Meli za Iran zimepita kwenye eneo hilo kwa mara ya kwanza tangu mwaka 1974.
Rais wa Urussi aonya kuhusu mapinduzi katika nchi za Kiarabu.
Moscow, Urussi - 22/02/2011.Rais wa Urusi ameonya ya kuwa mabadiliko ya kisiasa yanatotokea katika nchi za kiarabu yanaweza kuleta athali kubwa.
Rais Dmitry Medveded alisema " siafiki na jinsi viongozi wa nchi za magharibi ambao wamekuwa wana unga mkono mapinduzi ya kisiasa yanayo tokea katika nchi za Kiarabu, kwani yanaweza kuleta machafuko na kugawa nchi hizo ambapo matokeo yake yatakuwa mabaya kwa muda mrefu."
Akiongezaa " Inawezekana nchi hizi zikaja kutawaliwa na viongozi ambao wataleta maafa katika jamii. alisema rais Medved.
Maoni ya rais wa Urussi yamekuja kufuatia machafuko na mabadiliko ya yanayoendelea katika nchi za Kiarabu ambayo yameishitua dunia.

1 comment:

Anonymous said...

yap that is the type of leaderz african's we need to have with strong hold with their nation's......other african's leaders are perpet one's they are in power serving the western nation interest while their people are dying with hunger.disease and poverty in general.