Monday, February 14, 2011

Wasafiri wa anga wapata chombo kipya.

Wasafiri wa anga wapata chombo kipya.

New York, Amerika 14/02/2011. Kampuni ya ndege ya Boeing imezindua ndege mpya ambayo itakuwa hewani hivi karibuni.
Boeing imesema ndege "hiyo 747-8 Intercontinental itakuwa ikisafiri mwendo mrefu na waki huo ikitumia mafuta kiasi".
Ndege hiyo ambayo itakuwa na uwezo wa kuchukua abiria 467 ambao watakuwa wameongezeka kwa abiria 51 tofauti na ndege ya sasa 747.
Serikali ya Algeria yafuta amri ya dharula.
Algiers, Algeria 14/02/2011. Serikali ya Algeria imetangaza kusimamisha amri ya dharula ambayo ilikuwa imewekwa kwa kipindi cha miaka kumi na tisa.
Waziri wa mambo ya nchi za nje Mourad Medelci amesema " serikali imeamua kutoa amri ya dharula kama ilivyo haidiwa na rais Abdelaziz Bouteflika hiv karibuni."
Amri ya dharula iliwekwa mwaka 1992.
Kuondolewa kwa sheria hii imekuja baada ya serikali kuwa na wakati mgumu hasa kutoka kambi za nyama pinzani.

No comments: