Saturday, February 12, 2011

Rais wa Misri Hosni Mubaraka ajiudhuru urais.

Rais wa Misri Hosni Mubaraka ajiudhuru urais. Kairo, Misri - 12/02/2011. Sherehe, shangwe vigeregere vilivyo andamana na vilio vilisikika nchi zima mara baada ya makamu wa rais wa Misri Omar Suleiman kutangaza ya kuwa rais Hosni Mubaraka amejiudhuru na kukabidhi madaraka mikononi mwa jeshi.

Akiongea kwa muda wa sekunde thelathini, makamu wa rais alisema " rais Hosni Mubaraka ameamua kujiudhuru na kuanzia sasa na amekabidhi madaraka yote kwa kamati itakayo ongozwa na jeshi."
Rais Hosni Mubaraka, ambaye ametawala Misri kwa miaka 30, amejiudhuru baada ya msukumo mkubwa kutoka kwa waandamanaji ambao walikuwa wanadai atoke madarakani.
Maandamano yaliyo mfanya rais wa Misri kuachia madaraka yamechukua siku kumi nane, na kusababisha maafa makubwa ja kijamii na kiuchumi.

No comments: