Thursday, February 24, 2011

Rufaa ya mwanzilishi wa WikiLeaks yakataliwa.

Rufaa ya mwanzilishi wa WikiLeaks yakataliwa.

London, Uingereza - 24/02/2011. Mahakama jijini London imetupilia mbali rufaa ya mwanzilishi wa mtandao wa Wikileaks ambayo inapinga kupelekwa kwake nchini Sweden ili kujibu mashitaka.
Jaji Howard Riddle alisema " tumuma zidi ya mshitakiwa ni za kisheria na zinatakiwa zijibiwe kisheria hivyo inatakiwa mshitakiwa akajibu mashitaka."
Akiongea baada ya hukumu mwanasheria wa mshitakiwa Julian Assange alisema " tutakata rufaa dhizi ya uamuzi huu."
Juliana Assange ambaye amekuwa shubiri katika jamii ya kidipromasia baada ya mtandao wake WikiLeaks kutoa siri za viongozi na mabalozi wanapo kutana kila mara.
Mahakama ya kimataifa ya muhukumu miaka 27 jela mkuu wa zamani wa Polisi wa Serbi.
Hague, Holland 24/02/2011. Mahakama ya kimataifa inayoshughulikia kesi za Yugoslavia imemuhukumu aliyekuwa mkuu wa polisi Serb kwa miaka zaidi ya miongo miwili.
Vlastimir Djordjevic alihukumiwa na baada ya mahakama kumkuta na hatia ya kushiriki machafuko na mauaji ya Kosovo Albania.
Akitoa hukumu jaji Kevin Parker alisema " unahukumiwa kifungo cha miaka 27 jela kwa kukutwa na makosa ya kuhusika na mauaji ya watu 724 wa Kosovo Albania na kuleta mgawanyiko wa jamii katika eneo hilo."
Vlastimir Djordjevic alikamatwa mwaka 2007 huko Montenegro maada ya kukimbia na mafichoni kwa muda wa miaka minne.

No comments: