Thursday, February 9, 2012

Viongozi wa Urusi na Ufaransa wajadili kwa simu hali ya Syria

Al - Shabab wajiunga  rasmi na Al Qaeda.

Mogadishu, Somalia - 09/02/2012. Kiongozi wa kundi la Al-Qaeda ametangaza rasmi kuwa kundi la AlShabab lililopo nchini Somalia limejiunga rasmi katika kundi lake.
Ayman al Zawahiri ambaye ni kiongozi wa mkuu wa Al Qaeda alisema " napenda kuwatangazia ya kuwa kaka zetu katika imani Al - Shabab wamejiunga rasmi na Al-Qaeda na tutashirikiana nao kwa kila hali."
Kundoa la Al- Shabab limekuwa likiongoza mashambulizi zidi ya serikalia ya Mogadishu kwa muda mrefu na kusababisha kutokuwepo na amani katika nchi ya  Somalia

Sudani ya Kusini yatafuta mbinu mpya ili kusafirisha mafuta yake

Juba, Sudan ya Kusini - 09/02/2012. Serikali ya Sudani ya Kusini imetiliana sahihi mikataba na serikali za Ethiopia na Djibouti ili kuwezesha kujenga mabomba ya mafuta ambayo yatapitishwa katika nchi hizo.
Mikataba hiyo ni ya pili baada ya ya ule wa kwanza ambao serikali ya Sudani ya Kusini ilisini mkataba na serikali ya Kenya ili kuweza kujenga mabomba ya mafuta baada ya kutokea mgogoro na serikali ya Khartoum.
Serikali ya Sudani ya Kusini ilitangaza kusimamisha  uzalishaji wa mafuta kwa madai ya kuwa serikali ya Khartoum - Sudan kuzidisha kodi na kuiba mafuta. 
Kwa mujibu wa habari kutoka ofisi ya mawasiliano ya Sudani ya Kusini zinasema " ujenzi wa mabomba hayo utachukua miaka mitatu na kugharimu zaidi ya paundi za Kiingereza £ 3billion.

Viongozi wa Urusi na Ufaransa wajadili kwa simu hali ya Syria.
Moscow, Urusi - 09/02/2012. Rais wa Urusi amefanya mazungumzo na rais wa Ufaransa ili kujadili hali halisi ya kisiasa na machafuko yanayo endelea nchini Syria.
Katika mazungumzo hayo rais wa Urusi Dmitry Medvedev na Nikolas Sarkozy wa Ufaransa waliongea kiundani na kujadili ni kwa kiasi gani ahaadi zilizotolewa na  rais wa Syri Bashar al Assad wakati alipo kutana na waziri wa mambo ya nchi za nje wa Urusi nchini Syria.
Mazungumzo hayo yamekuja huku Urusi ikionya haitakuwa jambo la busara kwa nchi za nje kuingilia maswla ya ndani ya Syria, kwani ni ya wa Syria wenyewe.

Hali ya usalama nchini Syria yazidi kuwa tete.



Homs, Syria - 09/02/2012. Jeshi la serikali ya Syria limezidisha mashambulizi katika mji wa Homs na kusababisha maafa makubwa.
Mashambulizi hayo makubwa ambayo yameanza siku sita zilizo pita ikiwa ni moja ya nia ya serikali ya Syria kupambana na wale wote wanao leta vurugu katika mji wa Homs.
Habari zinasema " karibu maeneo ya makazi ya watu  katika mji wa Homs yamealiwa vibaya sana."
Nazo habari kutoka serikali ya Syria zinasema "Abdul Razzaq ambaye ni  mkuu wa jeshi la al Farouq jeshi ambalo lina pingana serikali ya Syria ameuwawa katika mashambulizi hayo."
Machafuko nchini Syria yalianza mwaka 2011 Machi, kufuatia upepo wa mageuzi ya kisiasa uliyo zikumba nchi za Kiarabu tangu kuanza kwa mwaka 2011.

No comments: