Monday, February 20, 2012

Waziri Mkuu wa Uingereza aombwa kupamabana na vilevi.

Waziri Mkuu wa Uingereza aombwa kupamabana na vilevi.
London, Uingereza - 20/02.2012. Wataamu wa afya nchi Uingereza wametahadhrisha madhara ya unywaji wa pombe katika jamii na kuonya yakua inasabaisha vifo vingi na kuhatarisha jamii.
Wataalamu hao wa afya ambao walifatilia na kufanya utafiti wa madhara ya pombe kwa jamii  walimwandikia barua Waziri Mkuu wa Uingereza David Cameron kutafuta mbinu mpya za kudhibiti unywaji wa pombe ambao umeongezeka katika jamii ya Waingereza.
Wakiongozwa na Profesa Ian Gilmore wataalamu hao walitoa ripoti inayosema "unywaji wa pombe umekuwa ukichangia kwa kiasi kikubwa katika magonjwa ya ini, msukumo wa damu, kupooza, magojwa ya moyo, kansa na magonjwa sugu kudumu na wanywaji wengi kuhusika na vurugu katika jamii."
Ripoti hiyo imekuja baadaya ya baadhi ya viongozi wa dini na wanasaiasa kudai serikali iangalie upya sheria za vinywaji vyenye vilevi, kwa ni idaiwa vilevi vimekua chanzo cha jamii nyingi kukosa amani.
 Waziri Mkuu wa Urussi ataka nguvu za kijeshi la nchi  ziongezwe.
Moscow, Urussi - 20/02/2012. Serikali ya Urussi imehaidi kuongeza nguvu za kijeshi, ili kuimarisha ulinzi wa nchi hiyo.
Waziri Mkuu Vladmir Putin alisema " nilazima kuimarisha nguvu za kijeshi ili kuweza kuilinda nchi yetu."
Kwamujibu wa habari zilizo patikana zinasema Urussi inatarajiwa kutumua zaidi ya £487billion ili kuimarisha maswala ya ulinzi wa nchi hiyo.
Putin ambaye anagombea kiti cha Urais wa Urussi mapema mwezi wa Machi mwaka huu alishawahi kuwa rais wa Urussi kabla ya kuchukua ka waziri mkuu wa Urussi.
China ya onya kuhusu ni ya  mashambulizi zidi ya Iran.
Beijing, China - 20/02/2012. Serikali ya China imepinga kitendo chochote cha mashambulizi zidi ya Iran na kudai yakuwa kutafanya eneo zima la Mashariki ya Kati kuwa na vurugu kumbwa.
Waziri wa mambo ya nje wa China Hong Lei alisema " gtumekuwa siku zote tunapinga vitendo vya kutishia vita  kati ya mataifa au taifa kwa taifa na huu ndoyi msimamo wetu."
Onyo hili kutoka serikali ya China,limekuja baada ya baadhi ya viongozi wa siasa nchini Marekani kudai hagtua za kijeshi itabidi zichukuliwe zidi ya Iran kwa kitendo chake cha kuendeleza mradi wa kinyuklia.
Hata hivyo serikali ya Iran imehaidi yakuwa kitendo cha nchi yoyote kuishambulia Iran basi Iran itajibu kwa nguvu zote mashambulizi hayo.

No comments: