Saturday, February 18, 2012

Maelfu waamuaga Whitney Houston.

Maelfu waamuaga Whitney Houston.

New Jersey, Marekani - 18/02/2012. Zaidi ya watu 1.500, ndugu, marafiki na jamaa wameudhuria misa ya mazishi ya mwana mama nyota wa muziki wa pop Whitney  Houston  48 ambaye alifariki hivi karibuni.
Katika kumwaga mwanamuziki Whitney Houston, wanamuziki maarufu duniani  akiwepo Stevie Wonder, waliimba nyimbo tofauti ikiwa ni heshima zao za mwisho kwa mwanamuziki huyo.
Whitney Haouston alikutwa amefariki dunia wiki iliyo pita katika hotel ambayo alikuwa amefikia katika jiji la Los Angeles.
Polisi nchini Senegal wapambana na waandamanaji.


Dakar, Senegal - 18/02/2012. Polisi wa kuzuia ghasia nchini Senegal wameshambuliana na wananchi katika jiji la Dakar baada ya kupinga agizo la serikali ya kutaka wasifanye maandamano.
Mashambulizi hayo ya polisi  yalitokea mara baada ya waandamanaji kuandamana kupinga kitendo  rais wa sasa wa Senegal kugombea kiti cha urais wa nchi hiyo kwa mara ya tatu.
Vurugu hizo zimekuja ikiwa zimebakia siku chache kabla ya  kufanyika uchaguzi wa urais ambapo rais wa sasa Abdoulaye Wade anagombania kiti hicho kwa mara nyingine.
Meli ya jeshi la Iran yavuka mfereji wa Suezi kwa mara ya pili.


Tehran, Iran - 18/02/2012. Meli za kivita za  jeshi la Iran zimeonekana katika bahari ya Mediteraniana na kuvuka mfereji wa Suez.
Mkuu wa msafara huo wa meli za kijeshi za Iran Habibollah Sayari alisema " niya ya safari hii nikuonyesha nguvu za  kiamani na urafiki."
Meli hiyo ya kijeshi inayojulikana kwa jina la  Shahid Qandi imekuwa ya pili tangu Iran kufanya mapinduzi mwaka 1979.
Msafara huo ambao haukutajwa kuelekea wapi,umekuwa wa pili kufuatia ule wa kwanza uliofanywa Februari mwaka jana.
William Hague  vita vipya vya baridi huenda vikaibuka.


London, Uingereza - 18/02/2012. Waziri wa mambo ya nje wa Uingereza ameeleza wasiwasi wake kuhusu maendeleo ya kinyuklia yanayo fanywa na Irani.
Willam Hague alisema " kutokana na mpango wa kinyuklia unaoendelea nchini Iran, kunaweza kuwa chanzo cha mashindano mapya ya vita baridi, na hii inazewa leta hatari katika jumuiya ya kimataifa.
"Ikiwa Iran itakuwa na uwezo wa kutengeza mabomu ya kinyuklia basi kutafanya nchi nyingine katika maeneo ya Mashariki ya Kati kujidhatiti na kuanza miradi ya kinyuklia."
Iran nchi ambao imekuwa ikitakiwa na nchi za Ulaya Magharibi na Marekani kuiachana na mpango wake wa kuendeleza maradi wa kinyukia imetangaza hivi karibuni kufanikiwa kuzalisha nguvu mpya za kinyuklia ambazo zitatumika katika utafiti wa kisayansi na kudai yakuwa haina mpango wa kutengeneza mabomu ya kinyuklia.
Nikolas Sarkozy kugombea tena kiti cha urais wa Ufaransa.
Paris, Ufaransa - 18/02/2012. Rais wa sasa wa Ufaransa ametamgaza hivi karibuni nia yake yakugombania tena kiti cha urais katika uchaguzi mkuu ujao mwaka huu.
Nikolas Sarkozy ambaye muhula wake wa kwanza wa urais unafikia ukingoni alitangaza kwa kusema "ikiwa kama sitagombani nafasi hii ya urais itakuwa kama kususa uongozi, hivyo nitagombania tena kiti hichi ili kukamilisha yale yote ambayo hatujayakamilisha kwa sasa"
Uchaguzi huo ambao unatarajiwa kufanyika mapema wakati wa mwanzo wa kipindi cha kiangazi mwaka huu, utakuwa ni mthiani mkubwa kwa rais Nikalas Sarkozy, kwani maoni ya kura bado yanaonyesha yakuwa bado anakazi kubwa ya kuwashawishi wapiga kura kumchagaua.


No comments: