Monday, February 13, 2012

Zambia yachukua ubigwa wa kombe la Afrika katika soka.

Zambia yachukua ubigwa wa kombe la Afrika katika soka.

Libreville, Gabon - 13/02/2012. Timu ya taifa ya Zambia imechukua ubingwa wa kombe la Afrika baada ya kuifunga Ivory Coast kwa penati 8 kwa 7.
Mechi hiyo ambayo ilichezwa huku kila timu ikitumia mbinu karibu zilizo fanana ili kutafuta ili bidi ichezwe kwa dakika 120 na baadaye kulekea kwenye penati na hatima yake Zambia kuibuka na ushindi.
Ushindi  wa Zambia nchini Gabon umekuja  na kuleta kumbukumbu kubwa kwa Wazambia kwani ufukwe wa bahari  wa nchi hiyo uliwapoteza viongozi na wachezaji wa timu taifa ya Zambia baada ya kupata ajali ya ndege.
Greeki yapiga kura kufanya mabadiriko ya  kiuchumi.

Athens, Ugiriki - 13/02/2012. Bunge la Ugiriki  limepiga kura na kupitisha mswada ambayo utaifanya serikali ya Ugiriki kubadili sheria ili kuimarisha uchumi.
Mswada huo ambao ulipitishwa utaiwezesha serikali ya Ugiriki kuweza kupata pesa kutoka  mfuko wa  jumuiya ya Ulaya.
Hata hvyo wakati wa mpango wa kupiga kura hiyo, zaidi ya watu 100,000 walikuwa mamesimama nje ya bunge hilo ili kupinga mswada huo, jambo ambalo lilisababisha vurugu kati ya waandamanaji na polisi wakuzuia ghasia.
Sudani ya Kusini na serikali ya Sudan zakubaliana makubaliano ya amani.

Adis Ababa, Ethiopia - 13/02/2012. Serikali ya Sudani ya Kusini na Serikali ya Sudan zimetiliana sahihi mkataba wa makubaliano kati ya nchi hizo  kuhusu  maeneo yaliyopo kati ya mipaka hiyo.
Mkataba huo ambao ulitiwa sahii na mkuu wa maswala ya usalama wa Sunadani ya Kusini Thomas Douth na  mkurugenzi mkuu wa usalama wa Sudan Mohamed Atta.
Mkataba wa makubaliaono hayo yalisainiwa mbele ya rasi wa zamani wa Afrika ya Kusini Thabo Mbeki ambaye ni mkuu wa majadiliano hayo.
Kwenye makubaliano ya mkataba huo wa nchi zote mbili unazitaka "Sudani ya Kusini na Sudan uheshimu mipaka ya nchi hizo mbili na kutoshabuliana kijeshi."
Kwa mujibu wa habari ziliz toka katika mkutano huo zimesisitiz aya kuwa kinacho fuata ni mazungumzo juu ya ugawaji na uzalishaji wa mafuta yaliyopo nchini humo.




No comments: