Wednesday, February 22, 2012

Rais wa Afghanistan aomba utulivu baada ya vitabu vya dini kuchomwa moto.

Rais wa Afghanistan aomba utulivu baada ya vitabu vya dini kuchomwa moto.

Kabul, Afghanistan - 22/02/2012. Rais wa Afghanistan amewataka wanachi wa Afghanistan kuwa watulivu na kutondelea na vurugu baada ya vitabu vya dini kuchomwa moto.
Rais Hamid Karzai alisema " naomba watu wausalama wasitumie nguvu, ila walinde usalama wa raia na vitu vyao."
Ombi hilo la rais wa Afghanistan limekuja baada ya kugundulika ya kuwa baadhi ya wanajeshi wa Marekani waliopo nchini Afghanistan walichoma vitabu vya dini Kiislaam - Koroani, baadaya ya kuvikusanya na kuondoka navyo kutoka kwenye jela moja  inayowashikilia wapiganaji wanahusika na kundi la Taliban wakati  waliopokuwa wakifanya uchunguzi ni mbinu gani zinatumika katika mawasiliano kati ya wapiganaji wa kundi la Taliban.
Serikali ya Marekani kupitia wakuu wa jeshi  imeomba msamaha kwa kitendo hicho kwa kusema  " tukio hilo siyo zuri na siyo msimamo wa jeshi la Marekani, kwani jeshi la Marekani linaheshimu dini zote."
Hata hivyo vuguvugu la maandamano kufuatia kuchomwa huko kwa Koroani bado linanendelea nchini Aghanistan kwa madai walio husika wawekwe mbele ya vyomba vya sheria.

Ugiriki yaopolewa na nchi wanachama.
Brussels, Ubeligiji - 22/02/2012. Jumuia ya nchi za Ulaya imekubalia kuipataia Ugiriki pesa nyingine ili kuinua uchumi.
Makubaliano hayo yalikuja baada ya Ugiriki kutimiza masharti ambayo ilitakiwa kuyatimiza.
Kufuatia kutimiza makubaliano hayo Ugiriki itapatiwa pesa kiasi cha dolla za Kimarekani $170billion ambazo zitaiwezesha serikali ya Ugiriki kuimarisha uchumi wake ambao ulikuwa umesha fikia kiwango cha kuporomoka.

Iran na IAEA zapishana mawazo.
Tehran, Iran - 22/02/2012. Wakaguzi wa maswala ya kinyuklia ambao wapo nchini Iran, wamekataliwa kutembelea eneo la kijeshi.
Mkurugenzi mkuu wa shirika linalo simamia maswala ya kinyuklia - IAEA International Atomic Energy Agency, Yukiya Amano alisema " tunasikitika ya kuwa wakaguzi wetu hawakuruhusiwa kutembelea eneo la Parchin ambalo linahusika na utaalamu wa maswala ya kijeshi."
Hata hivyo, mkuu wa maswala ya kinyuklia wa Iran, Ali Asghar Soltanieh alisema " tumeongea mambo mengi ya kujenga na natumaini tutakapo kutana tena tutaendelea kujadiliana kwa undani."
Wajumbe wa IAEA waliwasili nchi Iran kwa mara ya pili katika kipindi kisicho pungua mwezi mmoja ilikujadilia na serikali ya Iran katika maswala ya kinyuklia, jambo ambalo Iran imekuwa ikidai yakuwa inafanya maendeleo ya kinyuklia kwa ajili ya kukuza utafiti wa kisayansi.

Mji wa Baidoa nchini Somalia warudi mikononi mwa serikali.
Baidoa, Somalia - 22/02/2012. Majeshi ya Somalia na Ethiopia yamweza kuukamata mji wa Baidoa, ambao hapo mwanzo mji huo ulikuwa chini ya kundi la Al Shabab.
Baidoa mji ambao upo km 250 kutoka Mogadishu umekuwa chini ya kundi la Al Shabab na kusadikiwa kuwa kituo chao kukuu cha kupanga mikakati yao.
Masemaji wa jeshi la serikali ya Somalia Muhidin Ali alisema " majeshi ya serikali na Ethipoa yameweza kuutwaa mji wa Baidoa bila hata risasi moja kulia na maadua walikimbia mji kabla ya jeshi letu na la Ethiopia kuukamata mji huo, na watu wa mji huu wametukaribisha kwa shangwe."
Kukamatwa kwa mji wa Baidoa kumekuja  wakati Umoja wa mataifa umepitisha azimio la kuongeza msaada kwa jeshi la Umoja wa nchi za Afrika, ili kudumisha amani zaidi.

No comments: