Thursday, February 16, 2012

Aliyetaka kulipua ndege siku ya Krimasmas ahukumiwa kukaa maisha jela.

Aliyetaka kulipua ndege siku ya Krimasmas ahukumiwa kukaa maisha jela.
Detroit, Marekani - 16/02/2012. Mahakama nchini Marekani imetoa adhabu ya kukaa jela maisha kwa mshitakiwa ambaye alitaka kuilipua ndege iliyo kuwa ikielekea Marekani wakati wa siku ya Krismas 2009.
Mtuhumiwa huyo, Umar Farouk Abdul Mutallab ambeye alifanikiwa kuingia kwenye ndege ilikuilipua ndege hiyo ikiwa hewani kwa kutumia mabomu ambayo ailikuwa ameyavaa mwilini.
Mtuhumiwa huyo alikili kwa kusema " nilichukua mabomu ili kulipiza kisasi zidi ya serikali ya Wamarekani."
Hukumu hiyo ya kifungo cha maisha Jaji Nancy Edmunds baada ya kukutwa na hatia ya kutaka kuwauwa watu ambao walikuwepo kwenye ndege kuelekea Dertoit.

Iran yatangaza maendeleo ya kinyuklia.
Tehran, Iran - 16/02/2012. Serikali ya Iran imetangaza hivi karibuni kufanikiwa kutengeneza keki ubinjani ambayo itatumika katika kuimarisha nguvu za kufanya utafiti wa magonjwa.
Rais wa  Iran Mahmoud Hamedenejad alisema " Iran ipo tayari kushirikiana na nchi nyingine katika maswala ya kisayansi ili kupambana na magonjwa yanayo hatarisha maisha ya binadamu."
Uamuzi wa serikali ya Iran kutangaza maendeleo ya kinyuklia kumelaaniwa na nchi za Magharibi na Marekani na kudai ya kuwa "Iran haipo wazi katika maswala yake ya kinhyuklia."
Hata hivyo serikali ya Iran imekuwa ikikanusha madai hao, na kusema mpango wake wakinyuklia ni kwa aajili ya kukuza maendeleo ya kisayansi.

Umoja wa  Wajumbe wa  Umoja wa Mataifa wavutana juu ya Syria.
New York, Marekani- 16/02/2012. Mkutano mkuu wa Umoja wa Mataifa umelaani kwa pamoja matendo ya ukiukwaji wa haki za binadmu yanayo tokea nchini Syria na kupiga kura kupitishwa muswaada wa kutaka kusimamishwa mara moja vitendo hivyo.
Kura hizo zilizo pigwa 137 ziliaani  hasa vitendo vya serikali ya Syria chini ya rais Bashar al Assad didi ya 12 ambazo hazikubaliana na mswaada huo na kura 17 hazikupigwa.
Urusi, China na Iran zilipinga mswada huo kwa madai ya kuwa muswaada huo haukamilika kwani ulikuwa haulaani vitendo ya majeshi pinzani yanayopingana na serikali ya Syria.
Rais wa Syria Bashar al Assad amepitisha mswaada wakuundwa kwa katiba mpya itakayo husisha vyama vingi jambo ambalo vyama vya upinzani havikubaliani navyo.
Uamuzi wa kupigwa kura hiyo kumekuja baada ya mswaada mpya wa nchi za jumuiya za Kiarabu kutaka jitihada zaidi zifanyaike ili kuilazimisha serikali ya Bashar al Assad iachie madaraka na kuipisha serikali ya kidiplomasi itakayo chaguliwa na wananchi wa Syria.

No comments: