Friday, February 24, 2012

Somalia bado kitendawili kwa jumuiya ya kimataifa.

Hugo Chavez kufanyiwa upasuaji nchini Kuba.

Caracas,Venezuela - 24/02/2012. Rais wa Venezuela amewasili nchini Kuba ili kufanyiwa upasuaji.
Rais, Hugo Chavez 57 ambaye hapo mwazo alifanyiwa upasuaji ili kuondoa uvimbe wa kansa nchini Kuba, aliwaambia wanchi ya kuwa " kwa mara nyingine tena nipo vitani na nitashinda na kuishi vyema"
Wataalamu wa mambo ya kisiasa nchini Venezuela wamekuwa wanaulizana  kama rais Chavez ataweza kuongoza nchi tena kama akichaguliwa katika uchaguzi mkuu unaotarajiwa kufanyika mwezi wa Oktoba 2012.
Somalia bado kitendawili kwa jumuiya ya kimataifa.


Dadaab, Kenya - 24/02/2012. Wakimbizi wanao tokea Somalia wapo hatarini, baada ya  misaada ya kiutu iliyo tolewa kukaribia kuisha.
Dadaab ni kambi kubwa duniani ambayo ina wakimbizi zaidi ya 500,000 kutoka Somalia na inaaminika ya kuwa kuna wakimbizi ambao wameishi hapo zaidi ya miaka 15.
Kutoka kwa habari hizo kumekuja siku moja baada ya viongozi kukutana jijini London na kuweka mikakati mikubwa ya kupambana na makundi yanayo vuruga amani nchini Somalia.

No comments: