Tuesday, February 14, 2012

Mkuu wa jeshi wa Urusi aonyo kuwepo mashambulizi nchini Iran .


Izrael yailaumu Iran baada ya mashambilizi nchini India, Thailand na Georgia.
Tel Aviv, Izrael - 14/02/2012. Serikali ya Izrael imeilaumu serikali ya Iran kufuatia mashambulizi ya mabomu yaliyo tokea nchini India,Georgia na Thailand.
Heud Baraka ambaye ni waziri wa ulinzi wa Izrael alisema "mashambulizi yaliyo tokea yanaonyesha yakuwa Iran inafanya vita bubu zidi ya Izrael na mashambulizi haya ni ushaidi fika.
"Iran na Hezbollah wanashirikiana katika kuvuruga amani katika eneo la Mashariki ya Kati na dunia nzima."
Hata hivyo serikali ya Iran imekanusha kuhusika na mashamulizi hayo.
Mashamulizi zidi ya maofisa wa Kiizrael waliopo nchini India, Georgia na Thailand yametokea kwa kufuatana katika nchi hizo.
Hata hivyo Iran  ilishailaaumu Izrael kuhusika na mashambulizi zidi ya wanasayansi wake wanaohusika na maswala ya kinyuklia hivi karibuni ambayo yalitokea nchi Iran.
Na serikali ya Izrael ilikataa kuhusika na mashambulizi hayo.
Mkuu wa jeshi wa Urusi aonyo kuwepo mashambulizi zidi ya Iran.


Moscow, Urusi - 14/02/2012. Mkuu wa jeshi la Urusi ameonya yakuwa kuna kunampango wa kuishambulia Iran hasa kwenye maeneo ya viwanda vya nyuklia.
Meja Generali Nikolai Makarov alisema " Urusi inaangalia kwa makini swala hilo kwani upo uwezekano Iran kushambuliwa na uamuzi wa kufanya mashambulizi unaweza fanyika wakati wa kiangazi mwaka huu."
Mashambuli nchini Iran yamekuwa yakiongelewa na hasa kwa serikali ya Marekani kusema " uamuzi wowote juu ya Iran unaweza fanyika ikiwemo wa kivita."
Hata hivyo sertikali ya Iran ilishasema " ikiwa nchi yoyote itaishambulia Iran, basi Iran itajibu na majibu yake yatakuwa hayana mfano na maadhara yake yatakuwa makubwa."
Mvutano na malumbano ya kidiplomasia kati Iran na nchi za Magharibi zikiongozwa na Marekani umezidi kuongezeaka baada ya serikali ya Iran kutangaza yakuwa itafunga mfereji wa Strait Hormuz ikiwa itaona vikwazo vitahathiri uchumi wa Iran, jambo ambalo limezifanya nchi za Magharibi kupeleka maadhi ya maanuali zake za kijeshi karibu na eneo hilo.
Uingereza yafanya mazungumzo kumrudisha Abu Qatada nchini Jordan.
London, |Uingereza - 14/02/2012. Serikali ya Uingereza inafanya mazungumzo na serikali ya Jordan ili kupata huakika juu ya kurudishwa kwa mshukiwa Abu Qatada.
Kwa mijibu wa hamari kutoka ofise ya  mambo ya ndani zinasema "James Brokenshire, ambaye ni amewakilisha serikali ya Uingereza yupo nchini Jordan ili kuishawishi serikali ya nchi hiyo kukubali kmpokea Abu Qatada ambaye anshukiwa kuwa mtu hatari katika jamii ya Kiingereza.
"Serikali ya Uingereza itatumia kila minzi zilizopo ili kuwezesha kurudishwa kwa Abu Qatada."
Uamuzi wa serikali ya Uingereza kufanya mazungumzo na serikali ya Jordan juu ya Abu Qatada kumekuja  baada ya mahakama ya nchi wanachama wa jumuiya ya  Ulaya kukataa ombi la serikali ya UIngereza la kutaka Abu Qatada arudishwe nchini Jordan.
Mahakama hiyo ilisema " Kufuatia hali iliyopo nchini Jordan Abu Qatada hatapata haki na kesi yake haitakuwa halali kwani ushahidi utakao tumika ulipataikana kwa mateso na minyanyaso, ambayo inakwenda kinyume cha haki za binadamu na sherika za nchi wanachama wa Ulaya."
Abu Qatada aliachiwa kutoka jela kwa dhamana baada ya kukaa jela kwa muda mrefu bila kuhukumiwa  na ambaye anashukiwa kuwa mtu muhimu kwa kundi la Alqaeda na hasa kuwa mtu wa karibu na aliyekuwa mkuu wa kundi hilo hayati Osama bin Laden .
Taliban yakataa kukutana na serikali ya Hamid Karzai.

Kandahar, Afghanistan - 14/02/2012.  Kiongozi wa kundi la Taliban amekataa ya kuwa wanaweza kushirikiana na serikali ya Aghanistan kwa madai yakuwa serikali hiyo siyo halali.
Zabiullah Mujahidi ambaye ni msemaji wa kundi la Taliban alisema " hatuwezi kukaa  na kuongea na kundi la Taliban ambayo inaongozwa na Hamid Karzai.
Na hatujawahi kuulizwa wala kualikwa kuudhuria mazungumzo na serikali ya Karzai na hakuta kuwepo na uwezekano huo kwani serikali hiyo ni ya kibaraka na nikitu ambacho hakiwezekani kuongea na serikali ya kibaraka.
"Hata hivyo tumesha pata mwaliko wa kuongea na serikali ya Marekani, lakini hata hivyo kama  serikali ya Karzai atahusishwa basi hatutashiriki."
Mswada wa kukutanisha serikali ya Afghanistan inayo ongozwa na Hamid Karzai na kundi la Taliban ambao umekuwa ukiandaliwa na serikali ya Marekani ili kujaribu kusimamisha vita nchini Afganistan, vita ambavyo vimekuwa vikipigwana kwa muda mrefu sasa kati ya kundi la Taliban na serikali ya Afghanistan.


No comments: