Saturday, February 4, 2012

Urusi na China wapinga (veto) mswada wa nchi za jumuiya za Kiarabu kuhusu serikali ya Syria

Urusi na China wapinga (veto) mswada wa nchi za jumuiya  za  Kiarabu kuhusu serikali ya Syria.




New York, Marekani - 04/02/2012 - China na Urusi zimepiga kura ya veto kupinga mswada wa nchi wa jumuiya za Kiarabu uliyoletwa kwenye kikao cha kamati ya usalama ya umoja wa mataifa.
China  na Urusi nchi ambazo ni wanachama wa kudumu wa kamati ya usalama ya umoja wa mataifa wamepinga mswada uliyo wakilishwa na nchi za jumuiya ya Kiarabu ambao ulikuwa unataka kuilaani serikali ya Syria na kutaka kuwe na mabadililko ya uongozi nchini Syria.
Urusi imepiga kura ya veto, kwani katika mswaada huo haukuunganisha" kulaani vitendo ya vyama vya upinzani na majeshi yake ambayo pia yanahusika katika kuleta mvurugo wa amani nchini Syria."
Naye waziri wa mambo ya nje wa Urusi Sergie Lavrov anatarajiwa kuwasili nchini Syria ili kuzungumza na rais wa Bashar Assad.

Baraka Obama aionya serikali ya Syria.

Washington, Marekani - 04/02/2012. Rais wa Marekani ameitaka serikali ya Syria kuacha na kitendo chake cha kuvuruga amani pamoja na kuleta mauaji kwa wananchi wake.
Rais Baraka Obama alisema " Assad unatakiwa usimamishe vitendo vyote  vya mauji kwa wanachi wako, na unatakiwa uachie madaraka ili watu wafanye uchaguzi wa kumchagua kiongozi wao."
Hotuba hiyo ya Baraka Obama imekuja ikiwa kumebakia muda mchache kabla ya umoja wa mataifa kupiga kura kuhusu hali ya Syria.
Syria imekuwa nawakati mgumu wa kisiasa ulio andamana na mauji ya raia nchini humo.


Iran yaanza mazoezi ya kivita kwa mara ya pili mfurulizo.


Tehran, Iran - 04/02/2012. jeshi la Iran limeanza mazoezi ya anga na yanchi kavu ambayo ilikuwa imetangaza hapo wali.
Brigedia Mohammad Pakaour alisema "mazoezi hayo yatafanyika kwa wakati mmoja ili kuweza kujua ni kwa kiasi gani wanaweza kufanya kazi kwa pamoja."
Hii ni mara ya pili ya jeshi la Iran kutangaza kufanya mazoezi baada ya yale iliyo fanyanya hapo mwezi wa January.
Wakati huo huo wachunguzi wa mambo ya ulinzi wa Izrael wamedai yakuwa " Iran inazo siraha ambazo zinawezwa kurushwa hadi km 10,000 jambo ambalo siraha hizo zimnaweza kufika Ulaya na Marekani
Iran imekuwa ikitakiwa na Marekani na nchi za Jumuiya ya Ulaya  kuweka wazi swala lake la utengenezaji wa nyukli kwani zinazani ya kuwa Iran inampango wa kutengeneza siraha za kinyuklia.

No comments: