Monday, February 27, 2012

Wawili wakamatwa kwa kuwa na mipango ya mauaji ya Vladmir Putin

Ujerumani yakubali kuipa pesa Ugiriki.

Born, Ujerumani - 27/02/2012. Bunge la Ujerumani limepiga kura ya ndiyo kwa wingi ambapo itaruhusu kwa serikali ya Ujerumani kutoa pesa ili kusaidia Ugiriki.
Kura 496 ziilikubaliana na azimio ilo na 90 zilipinga.
Serikali ya Ugiriki inahitaji zaidi ya euro130 billion ili kuweza kuinua uchumi wake ambao upo njiani kuporomoka.

Wawili wakamatwa kwa kuwa na mipango ya mauaji ya Vladmir Putin.


Moscow, Urusi - 27/02/2012. Watu wawili wanshikiliwa na vyombo vya uslama baada ya kupatikana kuwa na njama za kutaka kumwua waziri mkuu wa Urusi.
Kwa mujibu wa habari zilizo patikana kutoka katika ofisi za usalama za Urusi na Ukraini " zinasema watu hao walikuwa wapepanga kufanya mauaji hayo na mashambulizi mengine mara baada ya uchaguzi wa urais unotarajiwa kufanyika hivi karibuni.
Watu hao wawili waliomo mikononi mwa vyombo vya usalama wanaaminika walipata amri hiyo kutoka kwa kiongozi wa kundi la Chechen Doku Umarov.

Wasyria  wakubali mabadiliko ya kisiasa na bursara za Kofi Annan zasubiriwa.


Damascus - Syria - 27/02/2012. Wananchi wa Syria wamepiga kura ya ndiyo ili kufanyika kwa mabadiliko ya mfumo wa kisiasa nchini humo.
Serikali ya rais Bashar al Assad, ili tisha kura za maoni ili kutaka kujua ya kuwa kama wananchi wa Syria watakubaliana namabadiliko ya mfumo mzima wa kisiasa.
Mataokeo ya kura zilizo pigwa  nchini kote zimeleta matokeo ya kuwa asilimia 90 ya wapigakura wamekubalia na mabadiliko ya kuwa mfumo wa sasa wakisiasa wa chama kimoja ubadilishwe.
Kufuatia matokeo hayo ya kura, Syria imefikia mwisho wa kuwa na chama kimoja na milango ya vyama vingi umefunguliwa rasmi.
Huku mabadiliko ya kisiasa yakiwa yapo njiani, katibu mkuu wa zamani wa Umoja wa Mataifa Kofi Annan aliteuliwa na katibu mkuu wa sasa wa umoja wa Matifa,  ilikusaidia kuleta suruhu za kisiasa nchini Syria.
Syria imekuwa katika hali ya vurugu za kisiasa kwa kipindi kirefu na kusababisha watu wengi kupoteza maisha kutokana na vurugu hizo.

No comments: