Tuesday, February 7, 2012

Urusi kushiriki katika mpango wa kuleta amani nchini Syria.

Malkia Elizabeth atimiza miaka 60 tangu kutawazwa kuwa Malkia wa Uingereza. 

London, Uingereza - 07/02/2012. Wanchi  na Malkia wa Uingereza wameanza kusherekea miaka 60 tangu Malkia Elizabeth kutawazwa rasmi kuwa Malkia baada ya kifo cha baba yake 1952 Mfalme George VI.
Katika kuadhimisha sherehe hizo Malkia  Elizabeth 85 alisema  "nawashukuru wananchi wote na wale wote waliomwezesha mimi na Prince Philips kuweza kuwepo, natumaini ya kuwa tutazidi kuwa pamoja wakati wa kutembelea sehemu tofauti nchini na nchi za nje."
Malkia Elizabeth anatarajiwa kufanya ziara katika nchi tofauti ikiwa ni moja ya kuadhimisha sherehe ya miaka 60 tangu kutwazwa kuwa Malkia wa Uingereza.

Urusi kushiriki katika mpango wa kuleta amani nchini Syria.


Damascus, Syria - 07/02/2012. Waziri wa mambo ya nchi za nje wa Urusi amewasili  nchini Syria ili kuongea na rais Bashir al Assad.
Sergei Lavrov alikutana na kuongea na uongozi wa rais wa Asad katika jitihada za kuleta amani nchini Syria.
Lavrov alisema " rais  Bashar al Assad amekubali kushirikiana katika kuhakikisha yakuwa amani inarudi nchini Syria na Urusi itakuwa mmoja ya wahusika katika mazungumzo hayo kwa kuwaunganisha viongozi wa upinzani kwani hii yote ni kwa niaba na manufaa ya Wasyria."
Nazo habari kutoka ofisi ya rais Asad zinasema " Uongozi wa serikali ya Syria upo tayari na unawakaribusha watazamaji kutoka nchi za jumuiya ya nchi za Kiarabu kuteta wajumbe ili waje kuangalia hali harisi."
Kuwasili kwa waziri wa mambo ya nje wa Urusi nchini Syria kumekuja wakati Marekani na Uingereza zimetangaza kuzidisha hatua zaidi katika kuhakikisha ya kuwa utawala wa rais Bashar al Assad unakomesha mauaji na ajitoe madarakani kufuatia maombi ya nchi za jumuiya ya Kiarabu.

Fataha na Hamas wakubali kushirikiana katika uchaguzi.


Doha, Katar - 07/02/2012.Viongozi wa vyama viwili ya kisiasa  vinayongoza sehemu tofauti za Wapalestina wamekutana na kukubaliana kuunguana ili kuaandaa uchaguzi mkuu ujao.
Viongozi hao wa vyama  Hamas na Fatah walikutana nchini Kuwait Doha na kukubaliana kwa pamoja ni kwa njia gani watashirikiana katika uchaguzi unao takiwa kufanyika hivi karibuni.
Katika kikao hicho rais wa  Palestina Mahamoud Abbas amechaguliwa kuongoza vyama hivyo hadi uchaguzi utakapo fanyika.
Waziri Mkuu wa Izrael Benyamin Netanyahu alisema " kitendo cha Fatah kushirikiana na Hamas kundi ambalo ni lakigaidi ni makosa makubwa ya kuvuruga mpango wa amani."
Vyama vya Hamas na Fatah vimekuwa na vinaongoza Wapelestina kwa maeneo tofauti. Hamas wamekuwa wakiongoza na kutawala Ukanda wa Gaza na Fatah wamekuwa wakiongoza West Bank.


Baraka Obama asiini mkataba wa kuwekewa vikwazo vya kibenki Iran.


Washington, Marekani - 07/02/2012. Rais wa Marekani amekubaliana na mswada uliopitishwa wa kuiwekea vikwazo Iran.
Rais Baraka Obama alitia sahiini sheria hiyoambayo itaifanya Iran kutokuwa na uhusiano wa aina yoyote kimabenki na benki za Marekani na vitengo vyote vinavyo husika katika maswala ya kifedha ili kuzuia kuinua na kukuza maradi wa kinyuklia ambao Iran unauendeleza.
Ofisi inayohsughulikia maswala ya kigeni ya Iran ilisema "vikwazo na kampeni ya Marekani imekuwepo na imekuwa haisaidii na hazitazimamisha nia yetu ya kuendeleza nia yetu ya kukua kisayansi hasa katika mpango wa nyuklia."
Vikwazo ambavyo vimewekwa kwa nchi ya Iran, vimekuja wakati Iran na Marekani zinapigana vita vya kidiplomasia kuhusu swala kinyuklia linalo enendelea nchini Iran.

No comments: