Tuesday, September 1, 2009

Walibya washerehekea miaka 40 ya utawala wa rais na kiongozi wao.

Walibya washerehekea miaka 40 ya utawala wa rais na kiongozi wao.

Tripol, Libya -01/09/09.Wanchi wa Libya waneanza rasmi kusherehekea miaka 40 tangu kiongozi na rais wao, Muammar Gaddafi, achukuwe madaraka.
Wakiwa katika mitindo mbalimbali wanachi wa Libya, wamekuwa wakionekana katika jiji la Tripol, wakishangilia kwa kila namna, wakati walipokuwa pamoja kwa muda wa masaa matatu na viongozi wengine kutoka nchi tofauti, kushangilia maonyesho yaliyo onyeshwa kwa ajili ya kukumbuka siku hii.
Maonyesho hayo, yalionyeshwa na makundi ya kiraia ,wanajeshi na kuonyesha historia ya Libya kwa ujumla.
Rais wa Libya Muaamar gaddafi, aliingia madarakani 1969, mara baada ya kuuangusha utawala wa kifalme ulio kuwa ukitawala wakati huo.
Picha hapo juu, anaonekana , rais wa Libya, Muammar Gaddafi, akishukuru Mola.
Picha ya pili, ni ya moja ya kundi lenye farasi, likitumbwiza kushangia miaka 40 tangu utawala wa rais, Muammar Gaddafi uwepo madarakani.
Picha ya tatu, anaonekana, rais wa Libya, Muammar gaddafi, kulia wakiingia mjini Tripol, mara baada ya kuuangusha utawala wa kifalme.
Wasiwasi ya kuwa jeshi la Ethiopia la ingia tena nchini Somalia.
Beledweyne, Somalia - 01/09/09. Jashi la Ethiopia,limeonekana ndani ya mipaka ya Somalia, kwa mujibu wa baadhi ya watu waliowaona wanajeshi hao.
Mamia ya wanajeshi hao wa Ethiopia, ambao wameingia nchini Somalia, na kukamata maeneo ya mji wa Beledweyne walifanikiwa bila kutupiana risasi na kundi la wapiganaji wanaopinga serikali ya Somalia.
Hata hivyo, AP, ilipata habari kupitia kwa mmjoja ya wakala wake ya kuwa wanajeshi wa Ethiopia, walikuwa wanaingia kila nyumba kutafuta siraha.
Hata hivyo,mkuu wa jeshi la Somalia, Muktar hassan Afrah, alikanusha madai hao ya kuwepo kwa jeshi la Ethiopia katika ardhi ya Somalia.
Waziri mkuu wa zamani wa Izrael kuingia kizimbani.
Jerusalem, Izrael - 01/09/09.Aliyekuwa aziri mkuu wa zamani wa Izrael, Ehud Olmert, amefunguliwa kesi ya kuhuusika kula rushwa.
Kesi hizo ambazo zina mkabili, bwana, Ehud Olmert, kupokea mchango kutoka kwa baadhi ya wadau wake wanaoishi nchini Amerika na kufanya maamuzi kinyume na sheria.
Hata hivyo, msemaji wa wa bwana Ehud Olmert, amesema ya kuwa kesi hizo hazina ushahidi, na kutokana na kashfa hizo za kutengenezwa zilimfanya ajiudhuru uongozi.
Waziri huyo mkuu wa zamani wa Izrael, Ehud Olmert, amekuwa waziri mkuu wa kwanza wa Izrael kushitakiwa.
Kwa mujibu wa wanasheria wa Izrael, wanasema ikiwa bwana, Olmert, atakutwa na hatia anaweza kuhukumiwa kifungo cha kwenda jela miaka kumi.
Picha hapo juu ni waziri mkuu wa zamania wa Izrael, Ehud Olmert, ambaye anakabiliwa na kesi ya ulaji rushwa.
Hakuna mazungumzo ya amani kwa sasa, mpaka Izrael isimamishe mpango wake.
West Bank,,Palestina - 01/09/09.Kiongozi mshauri wa mkuu wa uongozi wa Wapalestina, Saeb Erakat, amesema mazungumzo ya amani kati ya Wapaestina na Waisrael yatafanikiwa ikiwa seriakali ya Israel itakubali kutoka na kusimamisha utanuzi wa ujenzi katika maeneo ya West bank na Mashariki ya Jerusalem.
Erakat, aliyesema hayo siku ya jumatatu wakati alipokuwa akijibu maswali kuhusu hali halisi ya eneo zima la Mahsriki ya Kati na usalama wake.
Seab Erakat, aliendelea kwa kusema ya kuwa kwa sasa hakuna mipango ya mazungumzo kati ya rais wa Wapalestina ,Mahmoud Abbas na waziri mkuu wa Izrael,Binyamin Netenyau.
Picha hapo juu, anaonekana, Saeb Erakat, akiongea na waandishi wa habari kuhusu hali halisi ya usalama wa eneo zima la Mashariki ya kati.

No comments: