Tuesday, September 22, 2009

Amerika na Venezuela, kisa cha uhasama chawekwa hazarani.

Umoja wa Mataifa waanza kwa vishindo kukabiliana na mabadiliko ya hali ya hewa.

UN, Amerika - 22/09/09. Viongozi mbalimbali duniani, wamekutana leo kwenya ukumbi wa umoja wa mataifa kwa ajili ya kuangali upya ni jinsi gani wataifanya dunia kuawa sehemu ya amani na salama kwa viumbe wote.
Mkutano huo ambao uliitishwa na katibu mkuu wa UN,Ban Ki- moo,ilikuwahimiza viongozi hao kupambana na hali ya mabadiliko ya hali ya hewa duniani,hali ambayo katibu huyo alisema ipo haja ya kuishughulikia haraka kabla hali haijawa mbaya.
Akikubaliana na hoja hiyo , rais wa Amerika, Baraka Obama,alisema ipo jhaja viongozi wote wa dunia, kushirikiana kikamilifu ili kukabiliana na hali hii ya hatari, ambayo ikifanikiwa kutushinda basi hatutaweza tena kuikabili.
Picha hapo juu, anaonekana, rais wa Amerika, Baraka Obama, akihutubia viongozi, walioudhulia mkutana kujadili hali ya hewa duniani inavyo badilika kuelekea pabaya.
Picha ya pili anaonekana,katibu wa UN, Ban Ki moon, akimkaribisha, rais wa Amerika, Baraka Obama kuhutubia viongozi walilio udhulia mkutano kujadili hali mabadiliko ya hali ya hewa duniani.
Picha ya tatu, wanaonekana viongozi wa mbalimbali wakiwa wameka katika ukumbu wa mkutanao wa UN, huku wakimsikiliza rais, Baraka Obama.
Rais , Obama, awataka viongozi wa Izrael na Palestina kufanya uamuzi wa busara.
New York, Amerika - 22/09/09.Rais wa Amerika, Baraka Obama, amewataka viongozi wa Izrael na Palestina kufanya uamuzi wa busara na kwa makini ili kuleta amani.
Rais, Baraka Obama,aliyasema hayo wakati alipo kutana na viongozi hao, waziri mkuu wa Izrael, Binyamin Netanyahu na rais wa Wapalestina, Mahmoud Abbas, jijini New York, kujadili kwa undali hali ya amani kati ya Waizrael na Wapalestina.
Picha hapo juu, wanaonekana, rais wa Amerika, wa pili kutoka kushoto,waziri mkuu wa Izrael, Binyamin Netanyahu, kushoto,na rais wa Palestina, Mahmoud Abbas, kulia wakati walipo kutana leo jiji New York.
Amerika na Venezuela, kisa cha uhasama chawekwa hazarani.
Caracas, Venezuela - 22/09/09. Rais wa zamani wa Amerika, Jimmy Carter, Washington walijua yakuwa kulikuwa kuna mpango wa kuipindua serikali ya rais wa Veneuela, Hugo Chavez, mwaka 2002, na huenda ilishiriki kwa njia moja ama nyingine.
Jimmy Carter, alisema yakuwa hakuna shaka, mwaka 2002, serikali ya Amerika, ilikuwa inahabari kamili yampango huo, na ndiyo sababu, serikali ya rais, Hugo Chavez, ililaumu serikali ya Amerika na kuwa maadui wakubwa na serikali ya Amerika, iliyo kuwa ikiongozwa, rais George Bush.
Hata hivyo seriali ya Amerika, chini ya rais, George Bush, ilikanusha kuhusika na wala hawakuwa na habari za kutaka kuipindua serikali ya Venezuela.
Picha hapo juu, wanaonekana , rais wa zamani wa Amerika , Jimmy Carter kushoto,akiongea na rais wa Venezuela, Hugo Chavez,wakati walipo kutana hivi karibuni.
Usalama na amani wa Afghanistan bado kupatiwa jibu kamili.
Kabul, Afghanistan - 22/09/09.Kamando mkuu wa majeshi ya NATO, Stanley Mc Chrystal, amesema ya kuwa habari zilizo patikana katika vyombo vya habari, kuhusu hali halisi ya Afghanistan na usalama wake kwa raia utakuwa na wakati mgumu, kama hakutaongezwa na wanajeshi kupambana na kundi la Taliban, kwa umakini ni wa ukweli.
Kamando huyo,Stanley Mac Chrystal,aliilaumu serikali ya Taliban kwa kushindwa kudhibiti rushwa iliyo shamili nchini humo, na kwa sababu ya hali hiyo, inawafanya wananchi kutokuwa na imani na serikali.
Kamando, MC Chrystal, alisema yakuwa kuma hakutachukuliwa uamuzi wa busara, basi itafika wakati Taliban watakuwa ni wagumu kupambana nao.
Picha hapo, anaonekana, Gnl,Stanley McChrystal, akikagua maeneo ya kivita hivi karibuni.
Picha ya pili, linaonekana, jeneza la moja ya mwanajeshi wa jeshi la Amerika, akirudishwa nyumbani, mara baada ya kupoteza maisha wakati alipo kuwa katika mapambano na kundi la Taliban.
Izrael kuhaidi mbele ya Urussi, hakuna mashambulizi zidi ya Iran.
Moscow, Urussi - 22/09/09. Rais wa Izrael, Shimon Peres, ameihakikishia serikali ya Urussi, ya kuwa serikali ya Izrael,haitaishambulia Iran.
Uhakika huo ulitolewa mbele ya rais wa Urussi, Dmitry Medvedev, wakati alipo kutana na rais wa Izrael, ambaye alikuwa ziarani nchini Urussi.
Kwa kuongezea hayo,rais wa Urussi, Dmitry Medvedev,alisema yakuwa kitendo chochote cha kuishambulia Iran, kutakuwa ni kibaya na huenda kikaleta hali ya mashaka katika eneo zima la mashariki ya Kati.

No comments: