Wednesday, September 23, 2009

Viongozi wa dunia tukubali kuwajibika"Asema rais ,Baraka Obama"

Viongozi wa dunia tukubali kuwajibika" Asema rais, Baraka Obama" Umoja wa Mataifa,Amerika - 23/09/09.Rais wa Amerika, Baraka Obama, amewataka viongozi wa dunia, kukubali kuwa tayari na kukabiliana na mageuzi ya dunia ya sasa,kwani ina mapambano makubwa sana. Akiongea, rais Obama,alisema, nilazima kila kiongozi awajibike,kwani Amerika pekee yake haitaweza kutatua matatizo ya dunia nzima,ambayo yanasababishwa na matatizo yanayo ikabili dunia, na hatimayake kunapelekea kuwepo na watu wenyer itikadi kali na baadeye wanakuwa magaidi, wauwaji , wavurugaji wa amani na umasikini kuongezeka na hata kuharibu hali ya hewa na mazingira yake. Rais , Obama, alisema tangu kuchukua ofisi,yeye pamoja na uongozi wake wamejitahidi kupambana na ukweli wa hali halisi inayo ikabili dunia ya leo. Hii ndiyo hali halisi ambayo tunakabiliwa nayo. Kuhusu, hali ya amani ya Mashariki ya Kati, rais, Obama, alisema yakuwa uongozi wake utajitahidi kwa hali mali kuhakikisha amani inapatikana kati ya Wapalestina na Waizrael. Kwani wakatai umefika kukuzungumza bila kuwekeana vikwazo wala masharti, kwani wanaoumia ni wanachi wa Izrael na Wapalestina na siyo wanasiasa, "akijionyeshe yeye mwenyewe". Picha hapo juu, anaonekana rais , wa Amerika, Baraka Obama, akiwahutubia viongozi walioudhulia mkutano wa 64 wa umoja wa Mataifa jijini New York Amerika, ili kujadili hali ya dunia nzima inavyobadirika kimazingira na swala la kuwepo amani duniani kote. Rais wa Libya Muammar Gaddafi, ashambulia umoja wa matifa, "Adai mabadiliko ya kikatiba ya UN". UN,Amerika - 23/09/09. Rais wa Libya, Muammar Gaddafi, amelishambuli umoja wa Matifa kwa kusema ya kuwa linakwenda kinyume na katiba ya umoja huo. Akisisitiza, kwa undani, rais Gaddafi, alisema ya kuwa kamati ya usalama ya umoja wa matifa, haitakiwi kuwa baadhi ya nchi wanachama tu, bali kila nchi mwanachama lazima ihusishwe, kama hakutafanywa hivyo,ni kukiuka katiba ya umoja huu. Rais, Gaddafi, alisema yakuwa nchi ambazo zina viti vya kudumu, katika kamati ya usalama ya umoja wa mataifa , zina nyanyasa nchi ndogo na masikini,kwa kutumia kura zake za veto,na kwani katiba ya umoja huo,inasema ya kuwa nchi zote ni sawa ndogo hadi nchi kubwa. Akiongezea, rais Gaddafi, alisema yakuwa,inabidi umoja huu uundwe upya kikatiba ambayio itaipa kila nci hakisawa. Kuhuusu swala la amani mashariki ya kati,rais Gaddafi,alisema yakuwa Waarabu na Waizrael hawana uadui, bali ni mgongano wa kisiasa unao sababisha kutokuwepo na amani. Kwa kumalizia, rais wa Libya, Muammar Gaddafi, alisema yakuwa swala la kuleta amani duniani ni la kila kiongozi kuwajibika kikamilifu. Picha hapo juu, anaonekanana raia wa Libya, Muammar Gaddafi, awaaga viongozi wa nchi waliokuwa wakimsikiliza hotuba yake iliyo chukua saa moja na dakika 27,kuelezea kiundani wa UN. Lazima tutumize malengo tuliyo yaweka kwenye karne ya 21"Asema katibu mkuu" Umoja wa Mataifa,Amerika - 23/09/09.Katibu mkuu wa Umoja wa mataifa,Ban Ki moon,amefungua rasmi, baraza kuu la mkutano wa umoja wa mataifa la 64, na kusisitiza viongozi wa nchi zote kuungana kutimiza agizo la kupambana mabadiliko ya hali ya hewa na kuleta amani duniani, ili kufikia malengo ya karne ya 21. Katibu huyo, Ban Ki moon,ameagiza pia viongozi waasimamishe umwagikaji wa damu, huko mashariki ya Kati na Afghanistan,kupamabana na umasikini,kulinda haki za wanawake,kudumisha demokrasi,na kupunguza nguvu za nyuklia na bila kusahahu Somalia na Sudan. Picha hapo juu, anaonekanana, katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa, Ban Ki moon,akihutubia wakuu wa nchi walioudhulia mkutanao wa Umoja wa Mataifa wa 64, jijini New York.

No comments: