Saturday, September 19, 2009

Rais wa zamani wa Amerika aweka ukweli bayana.

Mitambo ya nyuklia ya Izrael yataikiwa ichunguzwe " Umoja wa Matifa wasema".

Viena Austria - 19/09/09. Shirika la Kimataifa linalo shughulikia ukaguzi wa siraha za nyuklia, limeitaka serikali ya Izrael, kuwaruhusu wachunguzi wa IAEA (International Atomic Egenegy Agency), kuchunguza mitambo yake na kuitaka nchi hiyo iingie kwenye mkataba wa na shirika hilo la la umoja wa mataifa.
Kwa mujibu habari kutoka umoja wa matifa, zinasema yakuwa kura zilipigwa siku ya ijumaa na kwa mara ya kwanza,mswada huo ulipata ushindi, wajumbe kutoka nchi za Kiaarabu walionesha furaha zao, kwa kuzingatia walikuwa wanajaribu kusukuma mswada huu upite kwa muda wa miaka 18.
Hata hivyo serikali ya Izrael,hakukubaliana na mswada huo.
Wakati huo huo,kuna habari yakuwa Iran inauwezo wa kutengeneza siraha zenye uwezo wa kinyukli, hii ni kwa mujibu wa uchunguzi uliofanywa na wachunguzi wa Umoja wa Matifa.
Kwamujibu wa UN, ni nchi tatu, ambazo hazina mkataba na IAEA, India, Pakistan na Izrael.
Picha hapo juu, ni alama ya shirka la kimatifa linalo shughulikia ukaguzi wa nyuklia na madhara yake, ambalo limekuwa na wakati mgumu kutatua mgogoro wa nguvu za nyukili duniani.
Picha ya pili, ni ya moja ya ndege za kivita za Izrael, ambazo zina uwezo wa kisasa wa kivita.
Picha ya tatu, inaonesha makombora yakitoka ardhini,hili ni moja ya mazoezi ya kijeshi ya jeshi la Iran, nchi ambayo imekuwa na mvutano na IAEA, kuhusu swala na nyuklia.
Amerika bado kupata jibu la kitendawili cha Izrael na Palestina.
Tel Aviv,Izrael - 19/09/09. Mjumbe wa serikali ya Amerika, ambaye anashughulika swala la kuleta amani kati ya Wapalestina na Waizrael, George Mitchell, ameshindwa kupata uhakika ya kuwa Izrael itasimamisha utanuzi wa ujenzi wa makazi,na kujua ni kwa jinsi gani, mazungumzo ya amani yata rudi kuzumgumzwa tena.
Kushindwa huko, kwa mjumbe huyo wa Amerika, George Michell, kuweka mikakati mipya ya kuwakutanisha viongozi wa upande wa Wapalestina na Izrael.
Kwa mujibu wa serikali ya Palestina, haitaweza kuendelea na mazungumzo, hadi hapo serikali ya Izrael, itakapo simamisha utanuzi ujenzi wa makao mapya katika eneo la West bank na Mashariki ya Jerusalem.
Picha hapo juu,anaonekana, mjimbe wa Amerika, George Mitchell,kushoto akiongea na waziri mkuu wa Izrael,Binyamin Netanyahu, kabla ya mjumbe huyo wa Amerika kurudi nyumbani.
Meli zenye takataka za sumu, kutafutwa baharini"Zimezamishwa makusudi"
Rome, Itali - 19/09/09.Serikali ya Itali imeanza uchungu wa kina,baada ya habari kuvuma ya kuwa kuna meli zenya uchafu na takataka za sumu zimekuwa zikizamishwa kwenye bahari ya pwani ya Kalabrian kwa makusudi na mamafia.
Kwa mujibu wa habari hizo , inasemekana kuana zaidi ya meli 32, ambazo zimezamishwa.
Akijibu swali hili, mkuu wa mazingira ya eneo la Kalabrian,Silvestero Greco,alisema yakuwa, habari hizi,zilitolewa na aliyekuwa mmoja ya mamafia hao Francesco Fonti, ambaye alikubali yakuwa yeye, alisha wahi kuhusika katika uzamishaji wa meli moja yenye takataka za sumu.
Picha hapo juu, ni nchi ya Itali,nchi ambayo, uchunguzi unafanywa kwa udani kujua meli zilizamishwa wapi na lini, ili kuopoa mazingira.
Picha ya pili, mkuu wa mazingi wa eneo la Kalibrian,Silvestero Groco,ambaye anajukumu kubwa la kuhakikisha maingira yakuwa ya usalama kwa binadamu na viumbe wengine.
Rais wa zamani wa Amerika aweka ukweli bayana.
Washington, Amerika - 19/09/09.Rais wa zamani wa Amerika,Jimmy Carter, amesema yakuwa wale wote, ambao wana kuongea vibaya kumpinga rais wa Amerika, Baraka Obama, wana fanya hivyo kutokana na chuki za kibaguzi,kwa kuzingatia , rais Obama ni abaasili ya Afrika ( Mweusi).
Jimmy Carter, aliyasema hayo, baada ya baadhi ya wananchi wa Amerika wenye msimamo mkali,kupinga kwa kashfa mipango ya rais, Baraka Obama ya kuinua hali za maisha na afya kwa wanchi wote wa Amerika.
Kufuatia, matamshihayo, pia rais, Baraka Obama, alikubaliana na mawazo hayo,kwa kusema ya kuwa anafahamu fika kuana, baadhi ya watu na viongozi wanapinga au wanampinga kuleta mabadiliko kutokana na rangi yake, na wengine wanakubaliana naye,hivyo ukweli ni kwamba kuja haja ya kuwepo na mabadiliko ya kimaisha, hasa kiafya kwa Waamerika wote, hiyo ndiyo moja ya melengo yake.
Picha hapo, anaonekana,rais wa zamani wa Amerika, ambaye huwa asiti kusema ukweli pindipo akiona baadhi ya viongozi wanakwenda kinyume na maadili mazuri ya uongozi
Venezuela ya ikaribisha China.
Caracas, Venezuela - 19/09/09. Serikali ya Venezuela imetiliana imtetangaza ya kuwa imetiliana mkataba wa $US dolla 16 billion na serikalia ya China,mkataba ambao utaiwezesha serikali ya China, kuchimba na kutoa mfuta katika jimbo la Orinoco.
Mkataba huo,ulio sainiwa jiji Beijing, unahusisha pia makubaliana ya kuwa serikali ya China,itasaidia ukarabati wa na ujenzi wa barabara na nyumba.
Picha hapo, juu anaonekana , akimpiga busu,mmoja ya wanafunzi wakati alipo kwenda kutembelea eneo ambalo,China imepata mkataba wa kuchimba mafuta.

No comments: