Friday, September 4, 2009

Baadhi ya nchi wanachama wa G20,wavutana katika kurekebisha vipato vya mabenki.

Bingwa wa muziki wa pop apumzishwa kwa amani.

Los Ageles, Amerika - 04/09/09.Aliyekuwa bingwa wa kucheza na kuimba musiki wa aina ya pop,hayati, Michael Jackson ampumzisha (amezikwa) leo katika eneo la mstitu wa Glendale Lawn.
Mazishi hayo yalihudhuliwa na ndugu na jamaa wa karibu wa Maichael Jackson.
Mwanamuziki huyo, alifariki dunia baada ya kunywa mchanganyiko wa madawa kwa ajili ya matibabu.
Picha hapo juu,ni hayati, Michael Jackson, enzi za uhahi wake.
Picha ya pili ni ya Michael Jackson,akiwa na kundi zima ambalo walishirikiana kucheza katika albam ya Thriller, ambayo ilimpatia sifakubwa na kuiuza kwa mamillion ya dola za Kiamerika.
Picha ya tatu, ni ya wazazi wa Michael Jackson, kushoto ni mama yake Michael, Katherine na kulia ni baba yake Michael mzee Jackson, walipo kuwa kwenye maombi ya mazishi ya Michael Jackson.
Ukame na vita, sababu ya upungufu wa vyakula na huduma UN.
Nairobi, Kenya - 04/09/09. Ukame ambao umelikumba eneo la Afriak ya Mashariki, limesababisha mamillion ya watu kukusa mazao ya kutosha kwa chakula.
Kwa mujibu wa habari, kutoka Umoja wa Matifa, zimesema kukosekana kwa mvua za kutosha, ambayo ndiyo chanzo cha kilimo kwa watu wengi wa eneo hili la Afrika ya Mashariki, kumeleta matatizo haya ya uhaba wa mazao ya chakula.
Pia Umoja wa Mataifa, uliongezea ya kuwa vita vinavyo endela kwenye baadhi ya maeneo ya Afrika ya Mashariki, yanchangia kwa kiasi kikubwa ugumu wa utoaji wa huduma za usamabazaji wa nafaka na chakula.
Picha hapo, juu ni ya ramani ya Afrika ya Mashariki, eneo ambalo hali ya ukame inatishia maisha ya wakazi wake.
Vita zidi ya Taliban, raia wazidi kupoteza maisha yao.
Kabul, Afghanistan - 04/09/09.Zaidi ya wetu wapatao 80mepoteza maisha yao,na wengine kujeruhiwa baada ya jeshi la NATO, ilipo kuwa ikilishambulia magari mawili,ambayo yalikuwa yamebeba mafuta yaliyo tekwa nyara na kundi la wapiganaji wa Taliban.
Mashambulizi hayo yalifanyika mapema alfajiri, katika cha Omar Kheil, maili 15 kutoka Kunduz.
Hata hivyo, NATO, imesema itafanya uchunguzi kuhusu mashambulizi hayo ambayo yamepoteza maisha ya raia, lakini NATO, ilisema tena kwa kusisitiza ya kuwa ilikuwa ikishambulia wapiganaji wa Taliban.
Picha hapo juu, wanaonekana, baadhi ya raia wa kijiji cha Omer Kheil, wakiwa wanawaifadhi, raia wenzao ambao wamepoteza maisha, mara ya mashambulizi yaliyo lengwa kwa kundi la Taliban.
Nchi wanachama wa G20, zavutana katika kurekebisha kipato cha mabenki.
Brussels,Ubeligiji - 04/09/09. Mawaziri wa fedha wa baadhi ya nchi za Ulaya wamesema ya kuwa kipato zaidi ambacho walikuwa wanapata wafanyakazi wa banki na benki kwa zaidi ya mwaka lazima zisimamishwe.
Uamuzi huo, ulipendekezwa, kwa kuzingatia, dunia ilikumbwa na mtikisiko na mporomoko wa uchumi, kupitia uongozi wa mabenki kutokuwa chini ya uangalizi, wakati wa kuongeza kipato.
Wakiongea kwa pamoja , mara baada ya kukutana mawaziri hao wa fedha, kutoka nchi za Sweden, Fransi,Spain,Ujerumani,Itali,Luxemburg na Uholanzi, walisema ya kuwa, ongezeko la kipato,litolewe kwa kipindi fulani cha miaka,kwa kuangalia ufanisi wa kazi wa benki hizo.
Hata hivyo, Uingereza na Amerika,bado hazijahafikiana na mpango huo.
Picha hapo juu, wanaonekana, rais , wa Amerika, Baraka Obama, kushoto , waziri mkuu wa Itali, Silvio Barluskon, katikati,na rais wa Urusi, Dmitry Medvedev, wakiwa wamepiga picha ya pamoja , jijini London, Uingereza,mara baada ya kumaliza mkutano wa kuangalia ni jinsi gani,dunia itaokoka kutoka katika janga la kudondoka kwa uchumi, ambapo dunia nzima ilikuwa katika hali ngumu mapema mwaka huu.
Morroko na Libya uhusiano kuwa mashakani.
Rabat, Morroko, 04/09/09. Seriali ya Morroko ,imeitaka serikali ya Libya kutoa maelezo kwanini walimwalika kiongozi wa Sahara ya Magharibi katika sherehe ya kuadhimisha miaka 40 ya utawala wa rais Muammar Gaddafi.
Ujumbe wa Morroko, uliondoka katika sherhe hizo, ambao ulikuwa umeongozwa na waziri mkuu, Abbas El Fassi, ikiwa ini ishara ya kupinga kualikwa kwa kiongozi wa Polisario.
Hata hivyo mpaka hivi sasa, serikali ya Libya haijatoa jibu lolote kuhusu madai ya serkali ya Morroko.
Picha hapo juu, ya baadi ya wapiganaji wa Sahara ya Magharibi, ambao wamejitangazia uhuru wao wenyewe, jambo ambalo.serikali ya Morroko inalipinga vikali.
Korea ya Kaskazini yaitaarifu UN na mpango wake wa uraniam.
New York, Umoja wa Mataifa. 04/09/09. Korea ya Kaskazini, imetaarifu Umoja wa Matifa ya kuwa inakaribia kukamilisha hatua ya pili ya kuchuja madini ya uranium na kuwa nauwezo wakutengeneza bomu la nyuklia.
Kwa mujibu wa habari kutoka serikali ya Korea ya Kaskazini,zilisema yakuwa habari hizo zilitumwa kwenye Umoja wa Mataifa na kufika kwenye kamati inayo shughulikia usalama.
Kwa mujibu wa msemaji wa serikali ya Amerika Stephen Bosworth,alisema , kitendo cha Korea ya Kaskazini kufukia hatua hiyo ni lazima kutizamwa kwa unagalifu sana, nainabidi serikali ya Korea ya Kaskazini, ikatazwe isiendelea na mpango huo.
Mapema hivi karibuni, Korea ya Kaskazini, ilikataa kuendelea na mazungumzo yanayo husisha pande sita, ambapo pande hizo zilikuwa zina jaribu kuizuia Korea ya Kaskazini kuendela na mpango wake huo.
Picha hapo juu, ni moja ya mitambo ya Korea ya Kaskazini, ambayo inatumika kuchujia madini ya uraniam.

1 comment:

Anonymous said...

Hello my friend! I wish to say that this article is amazing,
nice written and include

approximately all significant infos. I would like to see more posts
like this.

Take a look at my web-site: mcslist com free classifieds