Nchi zenye nguvu za kukubaliana kupunguza siraha zake za nyuklia.


Hii ni mara ya kwanza kwa rais wa Amerika kusimamia mkutano wa kamati ya usalama ya umoja wa mataifa.
Akiongea hayo,mwenyekiti aliye simamia kikao hicho, rais wa Amerika , Baraka Obama, alisema yakuwa kwa kipindi cha miezi 12 inayo fuata, kutakuwa na kazi ngumu kutekeleza yale yote yaliyokubaliaka na viongozi wote wa dunia hasa kwanchi zile zenya siraha za nyuklia.
Kwa mujibu wa (IAEA) shirika linalo shughulikia maswala ya nyuklia.zina sema, nchi ambazo zina siraha za nyuklia, Urussi, Amerika, Ufaransa, Uingereza, Izrael, India na Pakistan.
Picha hapo ujuu, anaonekana, rais wa Amerika, Baraka Obama, akisikiliza kwa makini, wakati wa kikao cha kuzungumzia kupunguza nguvu za siraha nyuklia duniani.
Picha ya pili,inaonyesha ni kwa kiasi gani, siraha za nyuklia, zitakavyo athiri mazingira na kuleta madhara kwa jamii pindipo zikitumika.
Picha ya tatu, ni alama ya nguvu za nyuklia, nguvu amabzo zikitumika vibaya dunia huenda ikawa historia.
Wapalestina lazima wakubali taifa la Waizrael" Asema waziri mkuu Binyamin Netanyahu"mbele ya UN.

Hata, hivyo, waziri mkuu huyo wa Izrael, alisema ile hoja yakuwa mauaji ya Waizrael ya Holokosti haya kufanyaika ni aibu kwa wote amabo wanasema hayo, kwani ushaidi ndiyo huu" Hapo alikuwa akionyesha baadhi ya karatasi ambazo zilikuwa zimetumika au kuandaliwa na watu wa kundi la NAZI.
Vilevile, alilaumu, kamati la umoja wa mataifa inaloshughulikia haki za binadamu, kwa kutoa uamuzi kwa upendeleo.
Waziri mkuu, Binyamin Netanyahu,alimaliza kwa kusema,kwa uwezo wa Mwenyezi Mungu, amani itakuwepo.
Picha hapo juu, ni picha ya waziri mkuu wa Izrael, Binyamini Netanyahu,ambaye alihutubia umoja wa mataifa leo.
Rais wa Iran, azilaumu nchi tajiri na zenye nguvu.

Rais huyo wa Iran, alisema yakuwa, nchi hizi za Ulaya, zimekuwa zikitangaza kuwa lazima kuwe na demokras katika kila nchi, lakini zinakiuka misingi kamili ya maana ya demokrasi, na imefikia wakati kwa dunia kuyaeleza kiuwazi,pia kutokueleweka kwa misimamo ya nchi hizi za Ulaya zenye nguvu, kwa kuuleza vingine na kutenda vingine kinyume na waliosema bali kukaripia nchi nyingine na kuzitisha.
Akizungumzia, swala la nyuklia, rais wa Iran, alisema kunahaja ya kuangamiza siraha za kibaiolojia na siraha za kikemikali,na kuruhusu kuwepo na teknolojia inayo tokana na nyuklia kwa matumizi ya ya maendeleo ya sayansi.
Picha hapo juu, anaonekana, rais wa Iran, Mahmoud Ahmadinejad, akihutubia mkutano wa 64 wa umoja wa mataifa mapema jana.
No comments:
Post a Comment