Saturday, September 12, 2009

Watatu wakutwa na hatia ya kutakakulipua ndege hawani.

Watatu wakutwa na hatia ya kutakakulipua ndege hewani

London, Uingereza -12/09/09. Mahakama imewakuta na hatia raia watatu wa Uingereza, kwa kutaka kulipuandege za shirika la ndege la Amerika wakati zikiwa hewani.
Watuhumiwa hao, Abdullah Ahmed Ali ,28, Tanvir Hussain, 28, na Sarwar,29,walikutwa na hatia, baada ya watuhumiwa hao kutaka kutumia bomb-mafuta ili kulipua ndege hizo za shirika la ndege la Amerika.
Kufuatiwa, kugundulika kwa njama hizo, kulibadilisha mfumo mzima wa usalama na ukaguzi wa abiria kabla ya kuingia kwenye ndege tayari kwa safari.
Picha hapo juu, ni ya alama, na ndege ya shirika la Amerika, ambapo zingelipuliwa wakati zikiwa hewani na abiria wake.
Picha ya pili ni ya watuhumiwa,ambao walitaka kulipua ndege kwa kutumia bomb-mafuta.
Amerika na Izrael, bado kuafikiana katika ujenzi wa makazi.
Jerusalem, Izreal. 12/09/09 - Habari za kuaminika kutoka nyambo ya habari vya Izrael, vimesema ya kuwa waziri mkuu wa Izrael, amefanya ziara ya kisili nchini Urussi, ilikujadili hali halisi ya usalama wa Izrael
Ziara hiyo ya kisili, imefanywa kutokana na wasiwasi wa serikali ya Izrael na serikali ya Iran na mpango wake wa nyuklia.
Serikali ya Izrael, imepitisha muswada wakuendela kujenga makazi katika eneo West bank.
Kupitishwa kwa muswada huo, kunakiuka makubaliano yaliyo wekwa kati ya serikali ya Izrael, chini ya uongozi wa waziri mkuu, Benyamin Netanyahu, na serikali ya Amerika chini ya uongozi wa rais , Baraka Obama.
Uamuzi huo ilio pitishwa siku ya jumatatu,na waziri wa ulinzi wa Izrael, Ehud Barak,kwa kuruhusu kujengwa numba zidi ya 455, kwaajili ya makaazi ya Waizrael.
Hata hivyo, serikali ya Wapalestina imepinga vikali uamuzi huo,na kutaka usimamishwe mara moja, ili mazungumzo ya amani yaendelee.
Picha hapo juu, anaonekana, waziri mkuu, wa Izrael, Benyamin Netanyahu, ambaye inasemekana alifanya ziara ya kisili nchini Urussi.
Picha ya pili, ni ya rais wa Amerika kushoto, Baraka Obama,na kulia waziri mkuu wa Izrael, Benyamin Netanyahu,ambapo viongozi hawa wanamisimamo tofauti kuhusu swala la ujenzi wa makazi kwenye eneo la West Bank.
Picha ya tatu, niya moja ya jengo ambalo lipo kwenye ujenzi.
Kutokuwajibika viruzi, mkuuwa Polisi afukuzwa kazi nchini Kenya.
Nairobi, Kenya - 12/09/09. Rais wa Kenya , Mwai Kibaki, amemfukuza kazi. mkuu wa polisi, Mohammed Hussein Ali, kwa kushindwa kutekeleza majukumu yake vizuri.
Mkuu huyo wa polisi, ambaye amefukuzwa kazi, anashutumiwa kwa kushindwa kuweka mikakati ya kutosha, kupambana na hali ya usalama wa raia,na hasa wakati wa kipindi cha uchaguzi, hali ilikuwa mbaya sana, na zidi ya watu 1500, walifariki dunia, watu kukimbia miji yao na wengi kujeruhiwa, kutokana na mvutano wa kisiasa, na polisi ilishindwa kuitambua hali hiyo kabla, na haya yote yalitokea chini ya uongozi wake.
Hata hivyo, mkuu huyo wazamani, Mohammed Hussein Ali, alikanusha madai hayo yakuwa alishindwa kazi,balia alisema ya kuwa wakati wa kipindi chake ujambazi ulipungua kwa kiasi kikubwa, na mikakati mingine ilikuwa bado inashughulikiwa.
Picha hapo, juu anaonekana mmoja ya walinzi wa usalama wa raia, akivuta tairi la gazi, lisije likashika moto, baada ya wananchi kufanya maandamano kupinga hali halisi ya usalama wao. Picha ya pili, nia ya panga, moja ya siraha zilizo tumika wakati wa vurugu za uchaguzi, panga hilo linaonekana likiwa limekatishwa juu ua moja ya kisiki cha mti na mmoja ya vijana wanao leta vurugu na kwa mbali ni wananchi, wakiwa wanaangali kwa makini nini kitafuata.
Mvutano wa siasa, Lebanon, bado kuwa na serikali.
Beiruti,Lebanon - 12/09/09. Waziri mkuu wa Lebanon, Saad Hariri, amejiuzulu uongozi wake wa kuwa waziri mkuu wa nchi hiyi, baada ya kupata upinzani mkubwa kutoka kwa vyama vingine vya kisiasa.
Upinzani huo, umetokea wakati, Saad Hariri, alipo, pendekeza baraza la mawaziri,ambalo lilipingwa na vyama vya upinzani, kwa madai ya kuwa, vyama hivyo havikutaarifiwa ya kuwa, Saad Hariri, anatawakilisha majina ya mawaziri kwa rais wa nchi.
Picha hapo, juu,wanaonekana, rais wa Lebanon, Michel Suleiman kushoto,na kulia Saad Hariri, wakati walipo kutana kimazungumzo.
Jela mwezi mmoja, kwa kuvaa suruali kinyume na sheria.
Khartoum, Sudan - 12/09/09. Mahakama nchini Sudan, imemkuta ,bi Lubaba Ahmed al Hussein kuwa na makosa ya kuvunja sheria, kwa kuvaa suruari, na hivyo kumtoza faini ya kiasi cha $200 za Kiamerika au kwenda jela..
Hata hivyo , bi, Lubana alikataa kulipa faini hiyo na na mahakama ikaamua kumuhukumu kwenda jela mwezi mmoja.
Hata hivyo tangu bi, Lubana kutiwa hatiani kwa kuvaa suruali,kumeleta msisimko wa kisiasa, hasa nchi Sudan na kwa jumuia ya kimataifan kwa kutaka bi Lubana,ahachiwe huru, kwa kesi hii hiyo, inakiuka haki za binadamu na uhuru kwa wanawake.
Picha hapo juu, anaonekana,bi Libana, Ahmed al Hussein akitokea mahakamani, kusikiliza kesi yake na kupewa hukumu kwenda jela mwezi mmoja.

No comments: