Thursday, September 17, 2009

Ofisi za ulinzi za Umoja wa Afrika nchini Somalia zashambuliwa.

Hatujengi tena mitambo ya kurusha makombora ulaya ya kati, "asema rais Baraka Obama.

Washington, Amerika - 17/09/09. Rais wa Amerika, Baraka Obama, amefuta mpango wa serikali ya Amerika kujenga mitambo ya kurushia makombora ya kijilinda na mashambuli ya kijeshi ya aina yoyote katika nchi za Poand na Czech.
Akiongea hayo, rais, Baraka Obama, alisema ya kuwa vitisho vya vilivyo kuwa vimewekwa na serikali iliyo pita, havikuwa na usahihi ya kuwa Iran, inaweza shambulia masrahi ya Amerika yaliyopo katika nchi za Ulaya, ambazo ni wananachama wa NATO.
Hata hivyo, rais, Baraka Obama, alisema yakuwa mitambo mipya ya makombora ina ya SM3 itajengwa katika meli za kijeshi na baadaye kuwekwa katika moja ya nchi za NATO.
Kwa kusisitiza hayo, waziri wa ulinzi wa Amerika. Robert Gate, alisema yakuwa, serikali ya rais, Obama bado inalitilia maanani swala la Iran kuwa na mitambo ya kinyuklia, na hivyo hakuna haja ya kuwa na shaka,kwani mitambo mipya itakuwa na uwezo wa kila aina kupambana na kila shambulizi.
Kufuatia uamuzi wa serikali ya Amerika, kufuta mpango wa kujenga mitambo ya kurusha makombora katika nchi za Poland na Czech,nchi hizo zimesema zimesikitishwa na uamuzi huo wa serikali ya Amerika.
Picha hapo juu, anaonekana, rais wa Amerika, Baraka Obama,ambaye amefuta mpango wa serikali ya Amerika kujenga mitambo ya kurushia makombora ulaya ya kati.
Picha ya pili ni ya baadhi ya makombora, yakiwa yapo tayari kwa mashambulizi wakati wowote,lakini kwa sasa mitambo ya makombora hayo hayatajengwa tena ulaya ya kati.
Ofisi za ulinzi za Umoja wa Afrika nchini Somalia zashambuliwa.
Mogadishu, Somalia - 17/09/09.Mabomu yamelipuka katika ofisi za makao makuu ya jeshi la Umoja wa nchi za Afrika zilizopo nchini Somalia kwaaajili ya kulinda amani.
Kufuatia mlipuko huo, watu wapatao 11, wamepoteza maisha, wakiwemo wanajeshi 6, wa jeshi la Umoja wa nchi za Afrika na wengine 18 kujeruhiwa vibaya.
Akiongea kuthibitisha ya kuwa kundi la Al Shabab,mmoja wa msemaji wa kundi hilo alisema yakuwa kundi lao ndiyo lililo fanya mashambulizi hayo, kwani wanahabari ya kuwa baada ya mwezi wa Ramadhan kuisha,jeshi la umoja wa nchi za Afrika unapanga kulishambulia kundi hilo, wamelipa kisasi cha kuuwawa mmoja wa kiongozi wao Ali Saleh Nabhan, ambaye aliuwawa na jeshi la Amerika siku mbili zilizo pita, baada ya kutafutwa kwa muda mrefu, kwa kuhusika na mashambulizi ya hotel na ndege ya Izrael nchi Kenya.
Picha hapo juu,linaonekana, moja gari la jeshi la Umoja wa Afrika, ambalo lipo katika mzunguko kwa ajili ya ulinzi katika moja ya mitaa ya mji wa Somalia
Picha ya pili wanonekana wapiganaji wa kundi la Al Shabab, wakiwa mazoezi,kundi hili limekuwa linapingana na serikali ya Somalia kwa muda mrefu sasa.
Waathirika wa uchafu na sumu kupata fidia, kampuni ya mafuta yakutwa na hatia.
Abidjan, Ivory Coast - 17/09/09. Kampuni ya kuuza mafuta, ya Trafigura imekubali kulipa fidia kwa watu na jamii nzima iliyo athirika na uzembe wa makusudi kwa kutupa takataka za mabaki ya sumu katika ufukwe wa bahari ya Ivory Coast.
Kwa mujibu wa habari kutoka UN,Umoja wa Matifa,zinasema ya kuwa kuna ushaidi kamili ya kuwa kutokana na kumwaga uchafu huo katika ufukwe wa bahari wa Ivory Coast,watu wengi wameathirika kiafya na hata wengine kupoteza maishayao,kwani uchafu huo ulikuwa nasumu.
Uchafu huo ulimwagwa na meli ya shirika la Probo Kaola, baada ya kukusanya uchafu uliotokana na mafuta yaliyo chujwa kutoka kwenye viwanda vya kuchujia mafuta hayo vilivyopo nchi za ulaya.
Picha hapo juu, wanaonekana baadhi ya wataalamu wa mazingira wakimwaga dawa kuua sumu iliyo mwagwa na meli ya Probo Kaola katika ufukwe wa Ivory Coast.
Picha ya pili, anaonekana mama mmoja, ambaye aliathirika kutokana na sumu,iliyo mwagwa na meli ya Pobo Kaola.
Hamid Karzai avilaumu vyombo vya habari
Kabul, Afghanistan - 17/09/09. Rais wa Afghanistan, Hamid Karzai, ambaye anagombania tena kiti cha urais huo kwa mara ya pili, amezilaumu baadhi ya vyombo vya habari kwa kutoa habari zinazo haribu ukweli wa hali halisi ya uchaguzi wa Afghanistan.
Hamid karzai, aliyasema hayo leo, wakati alipo kuwa akingea na waandishi wa habari, kufatia ripoti iliyo tolewa na wasimamizi wa uchaguzi kutoka jumuia ya umoja wa Ulaya, ya kuwa kulikuwa na ukiukwaji wa sheria za uchaguzi, baadhi ya kura zipatazo million 1.5 zimekuwa na utata.
Hata hivyo, Hamid Karzai, aliwataka wanachi wa Afghanistan kuwa wavumilivu, kungoja matoke ya mwisho, kwani atashirikiana kikamilifu katika kuchunguza kama kulikua kuna ukiukwaji wa kupiga kura.
Picha hapo juu, anaonekana, Hamid Karzai,ambaye anaongoza kwa kupata kura nyingi katika uchaguzi uliofanyika nchini Afghanistan, lakini haliya ya ukiukwaji wa kupiga kura bado hakujamwakikishia ushindi kamili.
Hatimaye bunge la umoja wa Ulaya lapata rais.
Brussels, Ubelgiji - 17/09/09. Umpja wa Ulaya, umemchagua tena, Jose Manuel Barroso, kuwa rais wa umoja huo, kwa kipindi kingine cha miaka mitano.
Katika uchaguzi huo, Jose Emanuel barroso, alipata kura 382,ambazo zilitakiwa kuzidi nusu ya idadi ya wabunge, kura 219 zilimkataa, na wabunge 117, hawakupiga kura.
Matokeo ya uchaguzi huu, kumemaliza utata, uliokuwa umezingira umoja huu kwa muda wa miezi sasa.
Akiongea mara baada ya kuchaguliwa, Jose Emanuel Barroso, alisema ya kuwa atahakikisha ya kuwa umoja wa wa Ulaya unadumisha demokrasi.
Picha hapo juu, anaonekana, Jose Emanuel Barroso,ambaye amechaguliwa kuwa rais mpya wa umoja wa Ulaya kwa kipindi kingine cha miaka mitano.
Japan yapata waziri mkuu mpya.
Tokyo,Japan - 17/09/09.Wanchi wa Japan, wamepata waziri mkuu mpya,Yukio Hatoyama, ambaye ameshinda uchaguzi uliofanyika mwezi uliopita.
Akihutubia mbele ya wabunge, waziri mkuu,Hatoyama, alisema atadumisha uhusiano uliopo kati ya Japan na Amerika, na vilevile kuendeleza uhusiano bora na nchi majirani zake hasa China.
Picha hapo juua anaonekana, waziei mkuu mpya wa Janap, Yukio Hatoyama,akiongea mbela ya wabunge mara baada ya kuapishwa kuwa waziri mkuu.

No comments: