Thursday, September 3, 2009

Moja baridi au moja moto,kwa wiki ni afya kwa wazee.

Moja moto au moja baridi kwa wiki ni afya kwa wazee.

Viena,Uswis - 03/09/09. Wachunguzi wanao uhusika na uwezo wa mwandamu kufikilia na uwezo wa ubongo wamesema ya kuwa wazee ambao wamesha timiza miaka 60 na zaidi wanauwezo kuongeza uwezo wao wa kiubongo kufanya kazi ikiwa watakuwa wana kunya pombe kwa kiasi kidogo.
Kwa mijibu wa habari hizo, zilizo tolewa hivi karibuni, zimesema ugonjwa wa kupoteza uwezo wa kufikilia na mabadiliko ya tabia au Alzheimer kwa jina la kitaalam, huwa unawatokea watu ambao wamefikisha umri wa miaka 60 na zaidi, unaweza kupungua ikiwa mzee mwenye zaidi ya miaka 60, atakunywa pombe kwa kiasi kidogo japo mara moja kwa wiki.
Picha hapo juu ni moja ya kinywaji (ulabu) pombe, moja kwa wiki kwa wazee kuanzia miaka 60, ni afya ya kunywa ili kuweka sawa hali ya ufanyaji kazi wa ubongo.
Picha ya pili ni ya mikongojo,(fimbo za kutembelea ambazo hutumiwa na wazee wanapo tembea), kunywa moja baridi au moto, kwa wiki ni afya ya kuweza kukumbuka mkongojo ameuweka wapi.
Baadhi ya viumbe huenda wakatoweka wasema wana sayansi.
Alizona, Amerika, 03/09/09. Jopo la wanasayansi ambao, wanafuatili kwa makini na kuchunguza mabadiliko ya hali ya hewa duniani, wamesema ya kuwa uharibifu wa mazingira, unaofanywa na binadamu, utaendelea kuathiri kwa kiasi kikubwa mazingira, ikiwa hakuna hatua za haraka hazitachukuliwa.
Akiongea hayo, mmoja ya wanasayansi hao, Jonathan T.Overpeck. alisema ushaidi unaonyesha wazi ya kuwa viumbe vinavyo ishi katika eneo la Aktik,vinazidi athirika,na uenda baadhi vikapotea kabisa, kutokana na kubadilika kwa mazingira yao ya kila siku, ambayo yanasababishwa na kuongezeka kwa hali ya ujoto kwa kasi kubwa.
Picha hapo juu, wanaonekana, jopo la wanasayansi wakifanya uchunguzi wao, katika ziwa la Sunday, kusini magharibi mwa Alaska.
Kampuni madawa yatozwa faini baada ya kukiuka sheria za nchi.
Washington, Amerika - 03/09/09.Kampuni moja ya kutengeneza madawa ya Ujerumani, ijulikanayo kama Pfizer, imetozwa faini ya kiasi cha dolla za Kiamerika 2.3 billion, baada ya kukutwa na hatia ya kutangaza madawa,kuuza madawa, na kupewa wagonjwa kinyume cha sheria kwa kushirikiana na wauguzi.
Kwa mujibu wa habari kutoka serikalini, zilisema yakuwa kampuni ya Pfizer, ilifanya vitendo hivyo bila ya kuwa na kibali cha serikali.
Akiongea hayo, mwanasheria mkuu wa jiji la New York, Andrew Cuomo, alisema ya kuwa faini hiyo ni kihistoria katika nchi ya Amerika, kwa kampuni kulipishwa.
Picha hapo juu ni ofisi za kampuni ya Pfizer, kampuni ya kutengenaza madawa, ambayo imetozwa faini mara baada ya kukiuka sheria za Amerika.
Mtoto wa aliye kuwa rais wa Gabon, atangazwa mshindi wa uchaguzi wa rais.
Libreville,Gabon - 03/09/09. Polisi jijini Libreville, wamepambana vikali na wanachama wa vyama vya upinzani, mara baada ya matokeo ya uchaguzi kutangazwa ya kuwa mtoto wa aliyekuwa rais wa zamani wa Gabon Ali Bongo kutangazwa kuwa mshindi.
Ali Bongo, ambaye baba yake, alitawala Gabon kwa muda mrefu hadi kifo chake, alikuwa mmoja ya wagombea wa kiti cha urais, baada ya baba yake kuacha wazi nafasi hii ya kiti cha urais.
Kwa mujibu wa matokeo ya uchaguzi, Ali Bongo, ameshinda kwa asilimia 41.73. na kuwashinda wapinzani wake wote walio shiriki katika uchaguzi huo.
Picha hapo juu ni ya Ali Bongo, ambaye anatarajiwa kuwa rais wa Gabon,baada ya kushinda uchaguzi wa kugombea kiti cha urais.
Picha ya pili,wanaonekana, baadhi ya watu wakiwa wamesimama nyuma ya moshi, baada ya wanachama wa vyama vya upinzani, kufanya vurugu na kuchoma mataili moto na kuvunja vunja vitu ,kupinga matokeo ya uchaguzi.
Picha ya tatu, wanaonekana maafande wa kuzuia vurugu wa Gabon, wakiwa wamemzunguka mmoja ya waandamaji aliye katikati yao mara baada ya kuwekwa chini ya ulinzi.

No comments: