Tuesday, September 15, 2009

Mwandishi wa habari aliyetikisa dunia atoka jela.

Mwandishi wa habari aliyetikisa dunia atoka jela.

Baghdad, Irak,- 15/09/09. Mwandishi wa habari, Muntadhar Al Zeidi, ambaye aliukumiwa kwenda jela kwa mwaka mmoja baada ya kumtupia kiatu aliyekuwa rais wa Amerika, George Bush, ameachili huru , baada ya kumaliza kutumikia kifungo chake.
Akiongea na vyombo vya habari, Muntadhar, alisema ya kuwa alishindwa kujizuia kumrushia kiatu aliye kuwa rais wa Amerika, George Bush,kwani alikuwa anawakilisha wale wote aliopoteza maisha, na kuumia kutokana na vita vya uvamizi wa Amerika kwa nchi ya Iraq,ambapo kila alipo kuwa akimaliza kazi alikuwa anapata ndoto za ajabu kwa kuona mateso ya watu wa ambao alikikuwa anawasaidi wakati akiwa kazini kwenye kuripoti matukio ya kivita, na ndiyo maana akaamua ya kuwa njia moja ya kumuuga na kumwonyesha rais Busha ya kukwa uvamizi wake umeleta maafa makubwa kwa wanachi wa Irak, ni kumtupia viatu na kumtukana.
Vilevile, Muntadhar, alisema baada ya muda atajtaja majina ya wale wote walio hisika katika kumtesa wakati alipo kamatwa na alipo kuwa jela.
Mwandishi wa habari huyo, alisema ya kuwa aliteswa vibaya sana, na madai yaliyo tolewa na waziri mkuu, hayakuwa ya kweli ,na kudai ya kuwa kuna watu wengi ambao hawana hatia wapo jela bila kufikishwa mahakamani.
Na mwisho, Muntadhar al Zeidi, alihaidi yakuwa atajitolea kusaidia wale wote waliopata matatizo kutokana na vita japo hali ya usalama wake upo mashakani, kwani kuana makundi yanampango wa kumua.
Picha hapo juu,anaonekana,akirusha kiatu kuelakea alipo kuwa rais wa zamani wa Amerika, George Bush,kabla ya kukamatwa na walinzi, ili asileta maafa zaidi.
Picha ya pili, wanaonekana, rais wa Amerika George Bush, kushoto na waziri mkuu wa Irak, Nouri al Maliki,wakati walipo kuwa pamoja kuongea na waandishi wa habari, kabla ya mashambulizi ya viatu yaliyo fanywa na Muntadhar al Zeidi.
Picha ya tatu, anaonekana , Muntadhar al Zeidi , akiongea na waandishi wa habari, mara baada ya kumaliza kifungo chake.
Venezuela yazidi jiimarisha kijeshi.
Moscow, Urussi, 15/09/09. Serikali ya Urussi , imekubali kuikopa serikali ya Venezuela, zana zakivita zenye thamani ya dola za Kiameria billion 2.
Zana hizo za kivita, ambazo zitakuwa mizinga ya kutungulia ndege,vifaru na siraha nyingine za kiteknologia ya kisasa.
Makubaliano hayo yalifanyikia wakati wa viongozi wa serikali hizi mbili walipo kutana jijini Moscow wiki mbili zilizo pita.
Kufuatia, Venezuela, kupata siraha hizo kutoka Urussi, serikali ya Amerika, imesema kuongezeka kwa matumizi ya kununua zana za kivita kwa Venezulam kunaweza kuleta hali ya wasiwasi kwa nchi majirani.
Picha hapo juu, zinaonekana, moja ya zana za kijeshi za Kirussi, ambazo Venezuela, itakuwa mmiliki wa baadhi ya zana hizo.
Adhabu ya kuzini ni kupigwa mawe hadi ufe, bunge lapitisha sheria mpya.
Aceh, Indonesia - 15/09/09. Jimbo la Aceh, ambalo ni sehemu ya Indonesia, limepitisha sheria ya kupigwa mawe hadi kufa, ikiwa mtu amakutwa na hatia ya kuzini.
Kwa mujibu wa habari kutoka katika bunge la jimbo hilo,ambalo wakazi wake wengi ni waumini wa dini ya Kiislaam,sheria hiyo itakayo julikana kama "Qanun jinayat"ita wakuta wale wote wanao kwenda kinyume na dini,ikiwepo mashoga, na wele wanao anza kufanya mapenzi kabla ya wakati.
Sherii hii itachukua mkondo wake kutokana na kosa lilitendwa, kwa kupigwa viboko 100, kwenda jela miaka mingi na kupigwa mawe hadi kufa na sheria hiyo itaanza kufanya kazi siku ya 31 tangu kupitishwa kwake.
Hata hivyo mashirika ya kutetea haki za binadamu, wamepinga vikali sheria hiyo na kudai imekwenda kinyume na haki za binadamu.
Picha hapo, juu wanaonekana baadhi ya wananchi wa jinbo la Aceh, wakiowa mbele ya bunge kupinga kupitishwa kwa sheria ya Kwanum Jinayati.
Rais, Baraka Obama, mabenki lazima yafatiliwe kiungalifu.
Washingtone, Amerika - 15/09/09. Rais wa Amerika, Baraka Obama, amesema ya kuwa hali ya uchumi wa Amerika una ananza kukua, kazi zinaanza kupatikana kwa wanachi wa Amerika.
Rais, Obama , alisema yakuwa, kukua kwa uchumi wa Amerika, ni kukua kwa uchumi wa dunia nzima, na kuporomoka kwa uchumi wa Amerika, kuliathiri uchumu dunia nzima,hivyo chini ya uongozi wake hataruhusu tena kutokuwajibika kwa wafanyakazi katika sekta ya fadha, ambo ndiyo chanzo cha mporomoko wa uchumi uliotokea kwa kipindi cha mwaka mmoja uliopita.
Rais Baraka Obama, aliliomba bunge la Kongresi kupitisha miswaada yote aliyo ipendekeza.
Picha hapo juu, ni ya rais wa Amerika Baraka Obama, ambaye toka, achukue madaraka kama rais wa Amerika, amekuwa na kibarua kigumu cha kuinua uchumi wa Amerika, ili kuwezesha nchi hiyo kurudi katika hali yake ya kawaida ya kuongoza dunia.
Helkopta ya kijeshi yafanya mashambulizi ya ghafla.
Mogadishu,Somalia - 15/09/09. Wapiganaji wawili wa kundi la Al Shabab, wameuwawa, baada ya helkopta ya kijeshi kuwashambulia wapiganaji hao walio kuwa ndani ya gari.
Kwa mujibu wa watu walio ona tukio hilo walisema yakuwa wanajeshi kutoka kwente helkopta walishambuli gari hilo karibu na kitongoji cha Barawe.
Na baadhi ya watu wamesema helkopta hiyo ilikuwa ya Kiamerika.
Nalo kundi la Al Shabab, limekubali ya kuwa kumekuwa na mashambulizi yaliyo fanywa kwa wapiganaji wake, lakini halikutoa maelezo kamili.
Hata hivyo, msemaji wa serikali ya Amerika, hakuweza kukana wala kukubali wakati alipo ulizwa kuhusu mashambuli hayo.
Picha hapo juu, kwenye ramani, sehemu ya ramani yenye rangi udongo mwekundu ni ya ramani ya nchi ya Somalia nchi ambayo imekuwa katika hali ya utata wa kiusalama kwa muda mrefu sasa

1 comment:

Anonymous said...

[url=http://sapresodas.net/][img]http://vioperdosas.net/img-add/euro2.jpg[/img][/url]
[b]macromedia flash5 software, [url=http://sapresodas.net/]10 Advanced Mac FileMaker[/url]
[url=http://sapresodas.net/]cheapest virus software[/url] discount software for educators buy windows software online
software to buy tickets [url=http://vioperdosas.net/]free antivirus software for windows xp[/url] adobe creative suite 4 torrent
[url=http://vioperdosas.net/]academic software in[/url] Adobe Creative Suite 3
[url=http://vioperdosas.net/]price check software[/url] medical office billing software
academic library software [url=http://sapresodas.net/]oem software what[/url][/b]