Sunday, September 13, 2009

EU-Muungano wa nchi za Ulaya watembelea Zimbabwe.

Rais wa Izrael, apata nafuu. Tel Aviv, Izrael - 13/09/09. Rais wa Izrael, Shimon Peres, ametolewa hospital, baada ya kumaliza kufanyiwa uchunguzi wa afya yake na waganga. Rais, Shimon Peres,ambaye alidondoka jukwaani wakati alipo kuwa akiongea katika mkutano mjini Tel Aviv. Hata hivyo, mganga aliye mfanyia uchunguzi, rais, Shimon Peres, Dr Zeev Rothstein, alisema yakuwa rais sasa yupo katika hali nzuri na hakuna wasiwasi. Picha hapo juu, anaonekana, rais wa Izrael, Shimon,akiwa anaongea, kabla ya kuanguka jukwani wakati akiongea na wanachi mapema jana. EU - Muungano wa nchi za Ulaya watembelea Zimbabwe.

Harare,Zimbabwe - 13/09/09. Viongozi wa muungano wa Umoja wa Ulaya na serikali ya Zimbabwe wamekutana kwa mara ya kwanza tangu mwaka 2001.
Ujumbe huo wa muungano wa Ulaya, ulikuwa nchini Zimbabwe kwa muda wa siku mbili, ili kuangalia maendeleo ya kisiasa kati ya chama cha rais wa Zimbabwe, Robert Mugabe ,na chama cha waziri mkuu wa Zimbabwe, Morgen Tsvangirai ni kwa jinsi gani wanashirikiana kujenga na kuinua maendeleo ya wananchi wa Zimbabwe, baada ya kuwa na hali ngumu ya kiuchumi kutokana na vikwazo vya kiuchumi vilivyo wekwa na jumuia ya kimataifa kwa nchi ya Zimbabwe.
Picha hapo, juu anaonekana, rais wa Zimbabwe, Robert Mugabe,ambaye serikali yake imekuwa na mvutano mkubwa na jumuia ya kimataifa,akimkaribisha mmoja wa wajumbe wa muungano wa jumuia ya Ulaya walipo fanya ziara nchini Zimbabwe..

No comments: