Monday, September 28, 2009

Bi, Angel Markel, kuongoza usukani tena nchini Ujerumani.

Ndugu wawili ,Wakijerumani ndiyo waanzilishi wa makampuni za viatu maarufu duniani.

Furth, Ujerumani - 28/09/09.Kampuni ya viatu ya adidas na Puma, zimetimiza miaka 60 tangu zianzishwe nchini Ujerumani na watoto wa baba mmoja Adi Dassler na Rudolf Dassler.
Jina la Adidas,linatokana na jina la Adi Dassler.
Puma ilianzishwa mwaka 1948, na adidas mwaka 1949,ilianzishwa rasmi kama kampuni ya viatu
Hata hivyo, kufuatia kutokuelewana kwa ndugu hawa, ndipo kulipelekea kuanzishwa kwa kampuni mbili za Puma na adidas, kampuni ambazo ndizo zinazo uza viatu kwa wingi duniani.
Mamba atumiwa na mafia kama utimizi masharti yao.
Rome Itali - 28/09/09. Serikali ya Itali imesema ya kuwa, kundi la mamafia waliopo nchini Itali wamekuwa wakitumia mamba ili kuweza kufanya biashara zao.
Mmoja wa mamafaia hao, Antoni Cristofaro,alikutwa na mamba mwenye uzito kilogram 40,kwenye bustani iliyopo nyumbani kwake Napeles.
Kwa mujibu wa wataalamu wa mswala ya wanyama,walisema mamba huyo, anauwezo wa kuvunja mbavu za mtu kwa mng'ato mmoja tu.
Hata hivyo bado uchunguzi unaendelea ni kwa jinsi gani mamba huyo aliweza kutumiwa.
Picha hapo juu, anaonekana mmoja wa mamba, ambao wamekuwa wanatumiwa kutishia watu ili kufuata masharti ya mamafia.
Rais wa Ufaransa ashitakiwa na waziri mkuu wa zamani.
Paris,Ufaransa - 28/09/09.Waziri mkuu wa zamani wa Ufaransa, Dominique Villepin, amefungua kesi zidi ya rais wa sasa wa Ufaransa,Nikolas Sarkozy.
Mwanasheria wa waziri huyo wa zamani,alisema yakuwa,rais Sarkozy, alihusika katika kashfa ya kuaribu jina la bwana, Villepin inakwenda kinyume na sheria.
Hata, hivyo, kesi ambayo rais,wa Ufaransa anashitakiwa, hataweza kufikishwa mahamani kutokana sheria ya nchi ya kuwa rais, hawezi kufikishwa mahakamani hadi hapo, atakapo toka ofisini kama rais.
Picha hpo juu, wanaonekana,rais wa Ufaransa, Nikolas Sarkozy kushoto, akiongea na Dominique Villepin siku za nyuma walipokuwa bungeni.
Picha ya pili, ni aliyejuwa waziri mkuu wa zamani wa Ufaransa,Dominique Villepin, ambaye uhusiano na Nikolas Sarkozy umekuwa utatani.
Bi, Angel Markel ,kuongoza usukani tena nchini Ujerumani.
Berlin,Ujerumani - 28/09/09. Kansella wa Ujerumani, Bi, Angel Markel na chama chake CDU- Christian Demokrat Union wamshinda uchaguzi mkuu uliofanykia mapema jana jumapili, kuvishinda vyama vingine kwa kupata kura nyingi kwa asilimia 33.8,wakati vyama vya SD - Social Demokrat kilipata asilimia 23 na vyana vingine vilipata asilimia chini ya 20.
Akiongea mbele ya wanachama na adau wake , Bi,Angel Markel, alisema yakuwa wamefanikiwa kwa kiasi kushinda lakini bado kuna kazi ya kujenga serikali mpya na kutatua matatizo ya nchi. Kufuatia, ushindi huo, mama Angel Markel, atatakiwa kuunda ya mseto kwa kushirikiana na vyama vingine.
Picha hapo,wanaonekana, Bi, Angel Markel kulia akiwa na mume wake,wakiangalia kwa tabasamu wanachama na wadau waliokuja kusikiliza matokeao ambayo yamempa ushindi mkubwa chini ya chama chake cha CDU.
Iran yaichanganya jumuia ya kimataifa.
Tehran,Iran - 28/09/09.Serikali ya Iran, imejaribu makombora yake ya masafa marefu aina Shabab 3 yenye uwezo ya kwenda km , 2000 namakombora mafupi aina ya shabab 1 na shabab 2 ambayo yanaweza kwenda umbali wa km 300-700.
Makombora shabab 3 yenye uwezo wa kwenda zaidi ya km 2000, yameleta wasiwasi kwa nchi jirani, kwani makombora hayo yanuwezo wakupiga Izrael , baadhi nchi ulaya, nchi za jumuia ya Kiaraabu.
Uzinduzi wa makombora hayo ulipokelewa kwa shangwe nchi Iran, wakuu wa jeshi wamesema hii ni kwaajili ya ulinzi wa Iran.
Kufuatia majaribio hayo ya makombora,jumuia ya kimataifa imelaani kitendo hicho na kudai kinatishia aman katika eneo zima.
Picha hapo juu,linaonekana kombora,likianza kuruka kuelekea hewani kwa majribio.

No comments: