Saturday, September 12, 2009

Mamia waudhulia kumbukumbu ya 11/9/2001,"Siku ambayo Amerika ilibadilika".

Mamia wa udhulia kumbukumbu ya 11/09/2001,"siku ambayo Amerika ilibadilika".

New York, Amerika - 12/09/09. Rais wa Amerika Baraka Obama, ameudhuria kumbukumbu ya mashambulizi yaliyo fanyika katika jiji la New York, mwaka tarehe 11/09/2001,ambapo zaidi ya watu 3000, walipoteza maisha yao na wengi kujeruhiwa.
Mashambulizi hayo yaliyo fanywa na kundi la Al Qaeda,yalibomoa moja ya majengo makubwa yaliyo julikana kama,kama majengo ya WTC, ( WorldTrade Centre), ambamo ndani ya majengo hayo kulikuwa na maofisi maduka na shughulinyingine zilikuwa zikifanyika katika majengo hayo.
Katika sherehe hiyo, rais, Baraka Obama, alisema ya kuwa vita zidi ya Al Qaeda na washiriki wake bado inaendela na wale wote walioshirkia katika mashambulizi haya, wata letwa mbela ya sheria.
Picha hapo juu,anaonekana rais, wa Amerika, Baraka Obama, akiwasalimia, baadhi ya wanchi waliokuja kuadhimisha kumbukumbu ya mashambulizi ya 11/9.
Picha ya inaonesha jinsi gani ujenzi mpya unavyo endelea katika eneo lilishanuliwa na kundi la Al Qaeda miaka 9 (tisa) iliyo pita.
Picha ya tatu, no moja ya masaliyo ya majengo yaliyo aribika vibaya baada ya kushabuliwa na kundi la Al Qaeda mwaka 11/9/12001.
Picha ya nne, inaonyesha majengo ya WTC, ( World Trade Centre ) yakiungua mara baada ya kushambuliwa na ndege, zilizotekwa nyara na kundi la Al Qaeda.
Nyuklia, Iran yasema hapana na Korea ya Kaskazini kitendawili, wote wataongea na Amerika na washiriki wake.
Washingtone, Amerika - 12/09/09. Serikali ya Amerika, imesema ipo tiyari kuongea na serikali ya Korea ya Kaskazini, ili kujaribu kuirudisha, Korea ya Kaskazini, katika mkutano wa uanao zijumuisha nchi sita, ili kuendela na mazungumzo kuhusu swala zima la nyuklia.
Maelezo hayo, yalitolewa na mwakilishi wa serikali ya Amerika, katika swala la nyuklia la Korea ya Kaskazini, Philip Crowley.
Hata hivyo, Philip Crowley, alikanusha ya kuwa, uamuzi huo, hautabadilisha msimamo wa serikali ya Amerika katika swala zima la nyuklia ya Korea ya Kaskazini.
Wakati huo, huo, serikali ya Amerika na washiriki wake na serikali ya Iran, zimekubaliana kuanza mazungumzo ya pamoja , lakini Iran imekataa kuongelea swala la nyuklia na kudai ya kuwa mradi mzima wa nyuklia ni kwa ajili ya matumizi ya kuzalisha nishati kwa ajili ya maendeleo ya Iran.
Picha hapo juu, ni bendera ya nchi ya Iran, nchi ambayo imekuwa na msimamo mkali kuhusu mradi wa nyuklia unaoendlea nchini Iran.
Picha ya pili, ni bendera ya Kora ya Kaskazini na sanamu la Askari wa Korea, nchi ambayo ina ipa jumuia ya kimataifa vichwa kuuma kuhusu usiri wake wa nguvu za nyuklia.
Jiji la Kampala, hali ya usalama si shwari.
Kampala, Uganda - 12/09/09.Watu wapatao kumi wamepoteza maisha yao, baada ya vurugu iliyotokea kati ya maafisa wa uasalama na raia, ambao wana muunga mkono mfalme wao.
Vurugu hizo zilianza wakati , serikali, kumzuaia mfalme Ronald Muwenda Mutebi,ambaye ni mfalme wa kabila la Baganda, kutembelea baadi ya maeneo katika jiji la Kampala.
Kwa mujibu wa serikali, mfalme huyo, hataruhusiwa kutembela maeneo hayo mpaka baadhi za sheria zitakapo tekelezwa.
Hata hivyo wachunguzi wa mabo ya kisiasa ya Uganda,wanasema ya kuwa kabila la Baganda lina asilimia ya watu wengi nchini Uganda, hivyo ikiwa hakutakuwa na suruhisho, basi kuna hatari ya kukosa kura za Baganda, ambapo Baganda wengi walikuwa wanampigia kura rais Museven.
Picha hapo juu, wanaonekana, baadhi ya wanancchi wakiwa mikono juu, kujisalimisha kwa maafisa wa usalama, iliwaweze kuendele na safari zao.
Picha ya pili, yanaonekna baadhi ya magari yakiwa yameungua vibaya baada ya kuchomwa moto kutokana na vurugu jijini Kampala.

No comments: