Tuesday, January 4, 2011

Laurent Gbagbo na Alassane Ouattara wakubali kukutana.

Laurent Gbagbo na Alassane Ouattara wakubali kukutana.

Abidjan, Ivory Coast - 04/01/2011. Mgogoro wa kisiasa nchini Ivory Coast huenda ukapata njia muafaka mara baada ya rais wa sasa na mpinzani wake kukubali kukutana ili kuongea kiundani tofauti zao za kisiasa zilizo letwa tangu kutangazwa kwa matokeo ya kura za urais. Akiongea na waandishi wa habari, mwakilishi wa Umoja wa Afrika ambaye ni waziri mkuu wa Kenya Raila Odinga alisema, "Laurent Gbagbo na Alassane Ouattara wamekubali kukutana mara baaada ya kukutana na viongozi hao." Raila Odinga na baadhi ya viongozi wa ECOWAS wamekuwa wakifanya kila juhudi kuleta suruhisho la kisiasa kati ya viongozi hao, ili kuiepusha Ivory Coast na machafuko na vurugu ambazo huenda zikapelekea kuleta vita kati ya wadau wa Ouattara na Gbagbo. Picha hapo juu wanaonekana viongozi wa ECOWAS na mjumbe wa Umoja wa Afrika Raila Odinga kulia wakatiwalipo kutana Alassane Ouattara.
Rais wa Sudan ahahidi kuunga mkono matokeo ya kura za maoni.
Juba, Sudan ya Kusini - 4/01/2011. Rais wa Sudan ametembelea Sudan ya Kusini siku chache kabla ya kufanyika kura za maoni ambazo huenda matokeo yake ya kasababisha kuigawa Sudan.
Rais Omar Al Bashir alisema " ningependelea kuwepo kwa umoja wa wanachi wa Sudan. lakini ikiwa matokeo ya kura yatapelekea kugawa Sudan, basi nitakuwa wa kwanza kuwa kuunga mkono matokeo hayo."
Omar al Bashir aliyasema hayo mbele ya wabunge wakati alipo kutana nao mjini Juba.
Picha hapo juu anaonekana rais wa Sudan wakati alipowasili mjini Juba ili kuongelea hali halisi ya matokea ya kura ya maoni itakayo pigwa hivi karibuni.

No comments: