Odinga, Ouwattara na Gbagbo hakuna maelewano.

Raila Odinga ambaye alipewa jukumu la kusuruhishwa mgogoro huo wa kisiasa aliwaambia waandishi wa habari ya kuwa imekuwa vigumu kufikia muaafaka kati ya pande zote mbili za kisiasa.
Akisisitiza Odinga alisema "muda wa mazungumzo ya hiyari unazidi kuwa finyu."
Hata hivyo msemaji wa serikali ya rais Laurent Gbagbo alisema "hatutakubali tena kuongea na Raila Odinga kwani anapendelea upande mmoja wa bwana Ouawattara na hatuko tayari kumpokea."
Picha hapo juu anaonekana Raila Odinga akiongea na waandishi wa habari mara baada ya kumaliza mazungumzo na Laurent Gbagbo pichani kulia na Alassana Ouwattara pichani kushoto.
Amerika na China kushirikiana kwa karibu zaidi.

Washington, Amerika- 19.01/2011. Serikali ya Amerika na Uchina zimekubaliana kushirikiana katika usalama wa maswala ya kinyuklia na sekta za kibiashara.
Kufuatia mikataba hiyo China itanunua ndege za aina ya boingi 200 na kuwekeza nchini Amerika vitega uchumi katika kilimo,mawasiliano.
Wakiongea mbele ya waandishi wa habari marais hao walisema kukutana kwao kumeweka msingi mzuri ambao nchi zote mbili zitanufaika."
Picha hapo juu wanaonekana rais wa Amerika Baraka Obama kushoto na rais wa China Hu Jintao wakiwasalimia wanchi waliokuja kuwalaki kabla ya kuanza mazungumzo rasmi kati yao jinsi ya kushirikiana kwa ukaribu zaidi.
Watunisia watakiwa kuungana.


Mtoa siri za benki za Swisi ahukumiwa.

Zuriki, Uswisi - 19/01/2011. Mahakama jijini Zuriki imemkuta na makosa aliyekuwa mfanyakazi wa benki aliyehusika kutoa nyaraka za siri kwa Wikileaks ambazo zinaonyesha majina ya watu ambao wameweka pesa katika benki nchini humo.
Mshitakiwa huyo Rudolf Elmer alihukumiwa kwa kutozwa faini ya kiasi cha Swiss 7,200 ($7,505) na kuwa chini ya uangalizi kwa muda wa miaka miwili.
Akitoa hukumu hiyo hakimu alikataa ombi la mwasheria kwa upande wa mashitaka kwa kutaka adhabu ya kifungo itolewe kwa bwana Ridolf Elmer.
Rudolf Elmer alikubali makosa yake kabla ya hukumo hiyo kutolewa.
Picha hapo juu anaonekana Ridolf Elmer ambaye alikutwa na hatia ya kutoa nyaraka za siri za benki kwa mtandao wa habari wa Wikileaks.
Jumuiya za nchi za kiarabu za tahadhalishwa.

Sharm el Sheikh, Misri-19/01/2011. Viongozi wa nchi za Kiarabu wamekutana nchini Misri ili kutasmini hali halisi ya jumuiya hiyo na kujadili wimbi la magauzi ambalo linaelekea kuzikumba nchi za Kiarabu.
Amir Mussa ambaye ni katibu mkuu wa jumuia ya nchi za Kiaarabu waliwaambia viongozi wa nchi wanachama ya kuwa hali ya kiuchumi katika nchi hizo inabidi ziangaliwe kwa undani sana, na "inatakiwa kuwepo na mabadiliko ya kiuchumi kwa serikali hizo kuwekeza rasilimali vitega uchumi ilikuinua maisha ya wanchi wa nchi hizo."
Akiongezea Amr Mussa alisema "mapinduzi yaliyo tokea nchini Tunisia lazima ma yaangaliwe kama mfano kwa serikali za nchi hizo."Na aliwataka wanchi wa nchi za Kiarabu kuwa pamoja ili kujenga nchi zao na eneo zima kwa ujumla.
Picha hapo juu anaonekana rais wa Misri Hosni Mubaraka akipokea ujumbe toka kwa moja ya washuri na huku katibu Amr Muoussa, akiangalia kwa makini.
No comments:
Post a Comment