Friday, January 7, 2011

Al Shabab walaumiwa kwa kuzuia misaada ya utu.

Al shabab walaumiwa kwa kuzuia misaada ya utu. Mogadishu, Somalia - 07/01/2010. Serikali ya Somalia inalimaumu kundi la Al Shabab kwa kuzuia misaada ya kiutu ambayo inatolewa ja jumuiya ya kimataifa. Habari kutoka wizara ya mambo ya ndani ya nchi zinasema ' inakuwa vigumu kusambaza misaada ya kiutu kutokana na hali ya kutokuwepo kwa usalama kwa wafanyakazi wanaohusika katika kutoa misaada." Kwa mujibu wa Umoja wa Mataifa, Somalia ni moja ya nchi ambayo ilikubwa na hali ya ukame, kiasi cha kuhatarisha hata mifugo. Picha hapo juu inaonyesha ni kwa kiasi gani hali ya ukame ilivyo hasili maisha ya watu na na wanyama.

Mabalozi wa Kanada na Uingereza watakiwa kuondoka nchini Ivory Coast.
Abidjan, Ivory Coast - 07/01/2010. Rais wa Ivory Coast amewataka mabalozi wa Uingereza na Kanada kuondoka mara moja nchini humo.
Uamuzi huo wa uongozi wa Ivory Coast kuwafukuza mabalozi hao, umekuja mara baada ya serikali hizo za Uingereza na Kanada kuwataka mabalozi wa Ivory Coast waliopo katika nchi hizo "kuondoka mara moja."
Hata hivyo wakati uongoziwa rais Laurent Gbagbo unavutana na jumuiya ya kimataifa, mpinzani wake Lassane Ouattara ameitaka jumuiya ya ECOWAS kutumia nguvu za kijeshi kumwondoa madarakani rais Gbagbo.
Picha hapo juu ni ya rais wa sasa wa Ivory Coast, Laurent Gbagbo ambaye amekuwa anavutana na jumuiya ya kimataifa mara baada ya matokeo ya uchaguzi wa rais kutangazwa.

No comments: