Wednesday, January 12, 2011

Kesi ya Julian Assange yaanza kusikilizwa.

Kesi ya Julian Assange yaanza kusikilizwa.

London, Uingereza - 12/01/2011. Mwanasheria wa mwanzilishi wa WikiLeaks ameiambia mahakama ya kuwa mteja wake atahukumiwa kifo ikiwa atapelekwa nchini Amerika. Mwanasheria huyo, alisema " ikiwa Julian Assange atapelekwa nchini Sweden, basi kunauwezekano mkubwa wa mteja wake kupelekwa nchini Amerika na kuhukumiwa adhabu ya kifo." Julian Assange, ambaye anatakiwa nchini Sweden kwa kosa la kufanya mapenzi rubuni amekuwa anapinga na kuwa alifanya kitendo hicho kama kinavyo elezwa.
Picha hapo juu anaonekana Julian Assange,akielekea mahakamani kusikiliza kesi yake.
Mafuriko yazidi kuleta athari kubwa nchini Australia.
Brisbane, Australian - 12/01/2011. Maelfu ya wakazi wa mji wa Brisbane wamehama mji mara baada ya mji mzima kukumbwa na mafuriko ya kihistoria.
Anna Bligh, alisema "zaidi ya makazi 20,000 huenda yakakumbwa na mafuriko na kuwaacha wakazi wake bila kitu."
Hali ya mafuriko nchini Australia imekuwa ikeendelea kwa kasi na kusabababisha hasara kubwa sana kwenye maeneo ambayo yamekumbwa na mafuriko.
Picha hapo juu wanaonekana baadhi ya waokoaji wa huduma ya kwanza wakiwa ndiani ya boti tayari kutoa msaada.
Serikali ya Rebanon yavunjika.
Beiruti, Lebannon - 12/01/2011. Serikali ya Lebanon imevunjika baada ya washiriki katika serikali ya muungano Hezbollah kujitoa.
Kuvunjika huko kwa serikali kumekuja baada ya kuzuka mabishano makubwa jinsi ya kupiga kura ili kuunga mkono matokeo ya uchunguzi wa mauaji aliyekuwa waziri mkuu Rafik al Hariri
mwaka 2005.
Serikali ya Lebanon imevunjika wakati waziri mkuu wa Saad Hariri akiwa ziarani Amerika kukutana na rais Baraka Obama.
Katibu mkuu wa umoja wa Matifa Ban Ki-moon alisema " ningependa kuwataka Walebanon kutatua maswala yao kwa amani na huru na umoja wa mataifa upo pamoja nao."
Hadi kufikia sasa uchunguzi wa kessi hiyo na matokeo yake yamekuwa yakipingwa na kundi la Hezbollah kwa madai ya kuwa matokeo yaina yoyote yatakuwa ya kisiasa hivyo haita yatambua.
Picha hapo juu ni ya aliyekuwa waziri mkuu wa Rafik al Hariri ambaye aliuwawa na bomu lililolipuliwa na watuwasiojulikana.

No comments: