Uchumi wa dunia kujadiliwa tena Davos.
Davos,Swiss - 26/01/2011. Viongozi wa serikali, wafanya biashara,,wanasiasa na wanauchumi, wanakutana nchi Uswisi ili kujadili mpangilio mzima wa uchumi dunia. Mkutano huo ambao utachukua siku tano, unatarajiwa kujadili mbinu za kuinua uchumi baada ya mtikiso mkubwa wa uchumi ulio ikumba dunia miaka miwili iliyo pita.
Kwa mujibu wa wachunguzi wa maswala ya kiuchumi wanasema " inabidi katika mkutano huu viongozi, wanasiasa,wafanya biashara na wanauchumi watafute ufumbuzi wa kuinua uchumi na siyo kuweka ahadi ambazo zimekuwa ziki tawaliwa na mzunguko wa siasa na hai halisi ya kiuchumi.
Picha hapo juu ni mji wa Davos, ambao viongozi wa nchi tofauti, wafanya biashara, wanasiasa na wanauchumi wanakutana kujadili hai halisi ya uchumi duniani.
Tunis,Tunisia - 26/01/2011. Polisi wa kimataifa wameombwa kukamata aliye kuwa rais wa Tunisia, mkewe na washiriki wa karibu wa familia yake ili wajibu mashitaka mbele ya mahaakama.
New York, Amerika - 26/01/2011. Umoja a Mataaifa umeombwa kuchangia mbinu mbadala za kupambana na maharamia waliopo katika pwani ya Somalia hadi kufikia pwani za Afrika ya Mashariki na kuanzisha koti maarumu itakayo husika na kesi za kiaaramia. 
No comments:
Post a Comment