Tony Blair awekwa kiti moto tena
London, Uingereza - 22/01/2011. Aliyekuwa waziri mkuu wa Uingereza wakati wa vita vya Irak na kumtoa madarakani hayati Saadam Hussein ameojiwa kwa mara nyingine tena na tume ya uchunguzi wa mwenendo mzima wa vita vya Irak.
Tony Blair ambaye alikuwa waziri mkuu wa Uingereza, chini ya serikali yake alishirikiana na serikali ya Amerika iliyo kuwa ikiongozwa na rais George Bush na kumn'goa madarakani rais Saadam Hussein wa Irak.
Akiongea mbele ya tume hiyo Tony Blair alisema " nasikitika kwa kwa wale wote waliopoteza maisha au kuathirika kutokana na vita hivi." Na nilimwahidi rais wa Amerika ya kuwa kutakuwa bega kwa bega katika vita hivi kwani niliamini Saadam Hussein alikuwa kiongozi hatri kwa jumuia ya kimataifa."
Uingereza na Amerika kwa kushirikiana na washiriki wengine ziliongoza vita vilivyo vikia kungólewa madarakani kwa rais wa Irak, Saadam Hussein.
Picha hpo juu ni ya aliye kuwa waziri mkuu wa Uingereza Tony Blair ambaye aalikuwa akijibu maswali kutoka katika tume ya kuchunguza mwenendo mzima wa vita vya Irak.

No comments:
Post a Comment