Umoja wa Afrika wachanga pesa ili kusaidia maeneo yaliyo kumbwa na ukame.
Adis Abeba, Ethiopia - 26/08/2011. Viongozi na marais wa Umoja wa Afrika wamekutana jijini Adis Abeba na kubaliana na kutoa mchango wa fedha kiasi cha £215milioni ili kusaidia maeneo ambayo yamekumbwa na ukame katika bara la Afrika.
Akiongea katika mkutano huo wa kuchangisha fedha, katibu msaidizi wa umoja wa mataifa Asha Rose Migiro alisema " bado tunaitajika kutoa misaada kwa wananchi wengi ambao wamekumbwa na ukame ili kuzuia janga la vifo na kupoteza kizazi kijacho cha bara la Afrika, na uwezo tunao wa kuzuia hali hii isiendelee kama tukishirikiana."
Katika mkutano huo pia benki ya Afrika iliahidi kuongeza juhudi zake za kuimarisha uchumi kwa kuwekeza zaidi katika miradi itakayo leta maendeleo kwa wananchi.
Kufanyika kwa mkutano huo wakuchangisha pesa, umekuja baada ya mashirika ya kimataifa kudai ya kuwa "umoja wa Afrika hauja lipa kipao mbele swala la kame lililo likumba bara hilo."
Serikali ya Uganda yatupilia mbali hukumu ya vifo kwa mashoga.

Kampala, Uganda - 26/08/2011. Serikali nchini Uganda limetupilia mbali muswada wa kutaka mashoga na kwa wale wote ambao wanapenda kufanya mapenzi kijinsia moja kupewa adhabu ya kifo.
Waziri wa serikali za mitaa, Adolf Mwesige alisema " serikali inapinga kitendo hicho, na kwa sasa kunasheria za kutosha za kushughulikia swala hilo."
Mswada huo wa kuwapa adhabu kali mashoga na watu wenyekupenda kufanya mapenzi kijinsia moja ulipendekezwa na mwaka 2009 na mbuge David Bahati, jambo ambalo lilifanya dunia nzima kutupia mcho yake nchini Uganda ili kutetea haki za watu hao.
Hata hivyo asilimia 90 ya wananchi wa Uganda wanapinga tabia za mashoga.
Naye mmoja wa watu ambao wanaunga mkoo kutupiliwa mbali kwa muswada huo alisema " huu ni ushindi kwa aliye kuwa mtetezi wetu David Katto, ambaye aliuwawa katika harakati za kutete haki sawa kwa kila Mganda."
Hata hivyo habari kutoka bunge la Uganda zinasema, "rais Yoweli Museveni, aliwaambia wabunge yakuwa wapunguze munkali na swala la mashoga, kwani kuna mambo mengi ambayo yanatakiwa kufanywa katika kuinua maisha ya wananchi.
Mlipuko wa bomu watokea katika majengo ya ofisi za umoja wa mataifa.


Abuja, Nigeria -26/08/2011. Milipuko ya mabomu imetokea katika jengo ambalo kuna ofisi za umoja wa mataifa na kuleta maafa makubwa.
Kwa mujibu wa mashaidi walio ona tukikio hilo walisema" mlipuko huo ulitokea baada ya gari moja kuvuka kizuizi cha kuingilia katika jengo hilo."
Naye katibu mkuu wa umoja wa mataifa Ban ki - Moon amelaani kitendo cha kulipuliwa ofisi za umoja huo na muuaji wa kujitolea muanga kwa kusema " ni kitendo hambacho hakionyeshi nia njema kwa wale wote ambao wanajitolea kufanya kazi ya kusaidia jumuiya za kimataifa."
Kufuatia mlipuko huo katibu msaidizi Rose Migiro atawasili nchini Nigeria ili kuongea na viongozi serikali na kupata habari kamili kwa ajili ya kuziwakilisha kwa katibu mkuu wa umoja wa mataifa.
Naye msemaji wa polisi Yemi Ajavi alisema "watu kadhaa wameumia vibaya na wengine kupoteza maisha na inaonekana kama ni mauaji ya kujitolea muhanga na mpaka sasa bado tupo katika harakati za uokoaji kwani kuna baadhi ya watu bado wamekwama ndani ya jengo hilo."
Rais wa Nigeria Goodluck Jonathan amelaani kitendo hicho na kusema " serikali itafanya kila njia kuwakamata wale wote walio husika katika mashambulizi hayo."
Kundi linalo julikana kama Bokaharamu limedai kuhusika na ulipuaji wa ofisi hizo za umoja wa mataifa, na kusema " uhu ni mwanzo wa kujibu mashambulizi baada ya serikali kutuma jeshi lake katika eneo la Kaskazini la Borno na kuna watu 100 ambao wapo tayari kujitolea muanga." Alisema msemaji wa kundi hilo Abu Darda.
Mlipuko huu wa bomu katika ofisi za umoja wa mataifa ni moja ya milipuko ya mabomu ambayo imekuwa ikitokea nchini Nigeria ambapo hivi karibuni bomu lililipuka katika ofisi za makao makuu ya jeshi la polisi jijini Abuja.
No comments:
Post a Comment