Samuel Eto'o avunja rekodi ya dunia kuwa mchezi wa mpira wa miguu kwa kulipwa pesa nyingi.




Dagestan, Urussi 24/08/2011. Mchezaji maharufu wa mpira waamiguu wa timu ya taifa ya Kameroon na Inter Milan Samuel Eto'o amevunja rekodi ya duia kwa kuwa mchezaji atakeye lipwa pesa nyingi baada ya kusaini mkataba na timu ya Anzhi Makhachkala iliyopo katika jimbo la Dagestan.
Samuel Eto'o , ambaye ameshinda kombe la ligi ya vilabu bingwa vya ulaya wakati akichezea timu Barcelona na Inter Milan, anatarajiwa kupokea kiasi cha 28.8million kwa muhula baada ya kusaini mkataba wa miaka mitatu kuchezea timu hiyo.
Eto'o atakuwa anapokea kiasi cha 350,000 kwa wiki kuliko wacheza wengine maarufu dunia ambao ni Wesley Snijder anapokea 250,000 kwa wiki, Christian Ronaldo 210,000 na mchezaji bora wa dunia Lionel Messi 180,000.
Akiongea baada ya kusaini mkataba Eto'o alisema " napenda kuwashukuru wapenzi na viongozi wa Inter Milan kwa kuonyesha mapenzi na ushirikiano kwa kipindi chote nilipo kuwa mchezaji na mkazi wa jiji la Milani.
Mapambano ya kikabila kutishia amani Kusini mwa Sudani.

Juba, Sudani ya Kusini -24/08/2011.Shirika la umoja wa mataifa -UNMISS - linaloshirikiana na serikali ya Sudani ya Kusini-,limeonya ya kuwa mauaji ya kikabila bado yanaendelea katika jimbo la Jongle.
Katika ripoti iliyo tolewa na shirika hili zinasema " watu wa jamii ya Murle na Lou Nuer wamekuwa wakipigana katika harakati za kutaka kila jamii iwe na mifugo mingi jambo ambalo ilinatishia amani katika eneo hilo"
Ripoti hiyo imeongezea ya kuwa katika maeneo hayo "bado kuna uhaba wa mahitaji muhimu ya kijamii."
Hata hivyo habari kutoka serikali ya Sudani ya Kusini zinasema " eneo hilo limeanza kupewa kipao mbele na itachukua muda kukamilisha miradi yote kutokana na mazingira ya kijiografia."
Sudani ya Kusini iliundwa baada ya kura ya maoni ya kutaka eneo hilo lijitenge kutoka serikali ya Kartoum, na kujitangazia utawala wake hivi karibuni.
Muammar Gaddafi ahaidi kufa au kupata ushindi.

Libya, Tripol -24/08/2011.Kiongozi wa Libya amelihutubia taifa kwa kutumia redio, huku mahali alipo ajulikani baada ya jeshi la wapinzani kuchukua makazi ya kiongozi huyo ya Bab al Aziziya na karibu maeneo ya jiji la Tripol.
Kanali Muammar Gaddafi, alisema "tunapigana vita zidi ya wasaliti wa Libya na katika mapambano haya kuna mambo mawili kufa au ushindi, na kitendo cha mimi kutoka hapo Bab al Aziziya ni mbinu za kujipanga tayari kwa mashambulizi, kwani tulijua ya kuwa NATO walikuwa wanataka kushambulia eneo hilo."
Naye msemaji wa serikali ya Libya, Mussa Ibrahim, akisisitiza kwa kupitia TV kutoka eno lisilo julikana alisema " Libya itakuwa na mlipuko wa volkano, majivu na moto na tunauwezo wa kupigana kwa muda mrefu."
Hata hivyo viongozi wa serikali ya mpito wamedai yakuwa "Muammar Gaddafi ameshaangushwa na tunampango wa kuamishia ofisi zote jijini Tripoli muda si mrefu na tunaendelea kumsaka hadi tu mkamate na ndipo Walibya watakuwa huru."
Hadi kufikia sasa Muammar Gaddafi na familia yake awajulikani wapo wapi jambo ambalo bado lina leta mashaka kwa serikali ya mpito.
Makampuni ya mafuta kusuguana vichwa baada ya kuanguka kwa Gaddafi

Hali hii inakuja baada ya serikali ya mpito kutangaza ya kuwa itaaangalia mikataba yote iliyo wekwa na serikali ya Muammar Gaddafi.
Habari kutoka ndani ya serikali hiyo ya mpito zinasema, " makampuni yote ambayo yanatoka kwenye serikali ambazo hazikushiriki katika kuunga mkono kung'olewa kwa Gaddafi huenda mikaaba yao ikafutwa."
Kufuatia habari hizi baadhi ya serikali zilizo tiliana mikataba na serikali ya Gaddafi "zimeshaanza mikakati ya kutaka kulinda mikataba hiyo kwa kila hali."
Libya ni moja ya nchi yenye utajiri mkubwa wa mafuta na tangu kuanza kwa vita nchin humo bei katika soko la mafuta imekuwa ikiyumba.
No comments:
Post a Comment