Monday, August 22, 2011

Serikali ya Tanzania yaonya viongozi wanaoshiriki biashara ya madawa ya kulevya.

Serikali ya Tanzania yaonya viongozi wanaoshiriki biashara ya madawa ya kulevya.
Dar es Salaam, Tanzania - 22/08/2011. Serikali ya Tanzania imeonya yakuwa wale viongozi wa dini na serikali wanao tumia madaraka yao katika kufanya biashara ya madawa ya kuleva watakamatwa muda si mrefu.
Akiongea na waandishi wa habari, mkuu wa kitengo cha kupambana na madawa ya kulevya
Godfley Nzowa alisema "tumepata majina ya watu wanaohusika na biashara hizo na bado tunafanya kazi ya uchunguzi zaidi ili kuwakamata wahusika wate. Na kunabaadhi ya majina tuliyo nayo ni yaviongozi wa dini na serikali wanaohusika katika biashara hiyo haramu."
Akijibu shutuma hizo kiogozi wa kanisa Katoliki, Kadinal Polycarp Pengo aliomba serikali iwataje viongozi hao wa dini ili kuthibitisha ukweli huo na kujenga imani kwa wananchi.
Onyo hilo limekuja baada ya ripoti kutoka ofisi za umoja wa mataifa zinazo shughulika na kupambana na madawa ya kulevya kuelezea ya kuwa "eneo la Afrika Mashariki limekuwa nikitovu cha kupitishia madawa ya kulevya kutokea Pakistani na sehemu tofauti duniani na kuwa ndio biashara kubwa inayo fanywa na wafanya biashara wakubwa na kukuza uharifu katika nchi za maeneo haya."
Serikali ya Afrika ya Kusini kuwa mwenyeji mkutano wa hali ya hewa na mazigira.
Durban, Afrika ya Kusini - 22/08/2011.Idara inayoshughulikia haliya hewa na mabadiliko yake ya umoja wa mataifa imeaanza maandalizi ya mkutano utakao fanyika nchini Afrika ya Kusini kuanzia Desemba 4 mwaka huu.
Kwa mujibu wa habari zinasema, "mkutano huo utawakusanyisha wajumbe wapatao 20,000, viongozi na wakuuu wa nchi wapatao 100."
Mkutano huo ambao ni moja ya mikutano ya kujadili hali halisi ya mabadiliko ya hali ya hewa,utajadili mikakati ya kupambana na uharibifu wa mazingira unaofanywa duniani kote.
Jiji la Tripoli lazungukwa na milio ya risasi baada ya jeshi la wapinzani kuingia.
Tripoli, Libya 22/08/2011.Jeshi la kundi la upinzani linalo pingana na serikali ya Libya limeingia jiji Tripoli kwa mara ya kwanza na kukamata badhi ya maeneo katika jiji la Tripoli.
Msemaji kundi hilo la kijeshi Guma El- Gamati alisema " Wapiganaji wetu wanashikilia karibu sehemu zote za jiji la Tripoli na jeshi la serikali lina shikilia maeneo matatu ambayo ni hospital, kambi ya kijeshi na Rixo Hotel na baadhi ya wapiganaji wa jeshi la Libya wamekuwa katika mazungumzo ya kusalimu amri ili kujisalimisha kwa jeshi letu."
Na habari kutoka kwa kiongozi wa jeshi la upinzani zinasema " mtoto wa Muammar Gaddafi ,Saif al Islam Gaddafi amekamatwa na jeshi hilo la upinzani na sasa yupo chini ya ulinzi wao."
Hata hivyo hakuna habari kutoka serikali ya Libya juu ya kukamatwa kwa mtoto huyo wa Muammar Gaddafi, ila msemaji wa serikali Mussa Ibrahim alisema mashambulizi yalyofanywa siku ya jumapili yameua zaidi ya raia 1,00 na zaidi ya 5000 kujeruhiwa vibaya."
Kufuatia kuingia kwa kundi hilo la upinzani jijini Tripoli, milio ya risasi imekuwa ikisikika karibu kila eneo ndani ya jiji hilo.
Mapigano kati ya jeshi la kundi la wapinzani na serikali ya MuammarGaddafi yalianza mapema mwezi machi na hadi sasa yameshafikisha miezi sita.

No comments: