Tuesday, August 30, 2011

Zimwi la vita vya Irak bado la mwandama Tony Blair.

Zimwi la vita vya Irak bado la mwandama Tony Blair.
London, Uingereza - 30/08/2011. Waziri mkuu wa zamani wa Uingereza Tony Blair anakabiliwa na wakati mwingine mgumu baada ya aliyekuwa mkuu wa usalama wa MI5 kudai alimwonya kuhusu vita vya Iraq.
Blair anakabiliwa na wakati mgumu baada yaaliyekuwa mkuu wa usalama wa MI5 Baroness Manningham-Buller kusema ya kuwa alimtahadhalisha na kumtaka ashughulikie kwa ukaribu zaidi vita zidi ya kundi la Al Qaeda.
Manningham-Buller aliongea kwa kusema "nilimwonya nakumweleza ya kuwa kitendo cha kuimshambulia serikali ya Sadam Hussein kijeshi, kutafanya hali ya usalama wa nchi kuwa na matatizo na hasa kutaonekana kama kushambulia dini ya Kiislaam, na ingefaa tuelekeze nguvu katika kupambana na kundi la Al Qaeda ambalo lina maficho nchini Afghaistan, kwani Irak haikuwa tishio katika usalama wa Uingereza."
Barroness Manningam-Buller ambaye amestaafu kazi mwaka 2007, aliongezea kwa kusema "vita vya Irak vimevuga mkakati wa kupambana na kundi la AlQaeda."
Kufuatia kauli hiyo ya mkuu wa usalama wa MI5, kumefanya baadhi ya wanasiasa kuanza kuuliza maswali mengi kwanini Uingereza iliishambulia Irak.
Mke wa Gaddafi na watoto wake wakimbilia Algeria na wapinzani watoa onyo la mwisho.
Algiers, Algeria -30/08/2011. Mke wa pili wa aliyekuwa kiongozi wa Libya Muammar Gaddafi amekimbilia nchini Algeria pamoja na watoto wake.
Habari kutoka ofisi ya wizara ya mambo ya nchi za nje zimesema " Safia Gaddafi aliwasi saa 08:45 na watoto wake Aisha, Hannibal na Mohammed na tumewapokea kiutu jambo ambalo kila mtu anahitaji kupewa."
Mahmud Shammam msemaji wa serikali ya mpito alisema " kitendo cha Algeria kuipokea famila ya Gaddafi ni kinyume na matwakwa ya Walibya na tutaomba warudishe nchini Libya waje wajibu mashitaka ya kutumia mali ya umma vibaya."
Serikali ya Algeria ilikuwa na uhusuano mzuri na serikali ya Muammar Gaddafi kwa kipindi kilefu na mpaka sasa imekataa kuitambua serikali ya mpito ya Libya.
Wakati huo jeshi la serikali ya mpito limetoa onyo la mwisho kwa wanajeshi ambao wanamuunga mkono Muammar Gaddafi kusalimu amri au kuwatayari kwa mapambano ikifika siku ya Jumamosi.
Onyo ilo limekuja wakati jeshi la wapinzani likiwa limezingira mji Sitre ambao unasadikiwa kuwa kuna nguvu nyingi za kijeshi na nimji alio zaliwa Muammar Gaddafi.
Mahakama ya haki za binadamu yakataa maombi ya Kenya.
Nairobi, Kenya -30/08/2011.Rufaa ya serikali ya Kenya kwenye mahakama ya kutetea haki za binadamu imekataliwa na mahakama iliyopo nchini Uhollanzi.
Rufaa hiyo ambayo ilikuwa imeitaka mahakama ya Hague kusimamisha kesi zidi ya washitakiwa sita akiwemo makamo wa waziri mkuu, mawaziri , mmoja wa mkuu wa polisi na viongozi wengine waliohusika katika kuchochea machafuko baada ya matokeo ya uchaguzi mkuu kutangazwa mwaka 2007.
Kesi hiyo ina tarajiwa kuanza siku ya Alhamisi wiki hii, ambapo washitakiwa hao wanatakiwa kujibu mashitaka zidi yao kwa kuhusika na machafuko yaliyo sabaisha mauaji na mali nyingi kuteketea.
Kesi hiyo ilifunguliwa baada ya mwanasheria mkuu wa mahakama hiyo Luis Moreno -Ocampo kumaliza uchunguzi wake aliyo ufanya nchini Kenya baada ya machafuko kutokea.
Serikali ya Zimbabwe yamfukuza balozi wa Libya.
Harare,
Zimbabwe - 30/08/2011. Serikali ya Zimbabwe imemfukuza balozi wa serikali ya mpito ya Libya baada ya kutamka ya kuwa anaunga mkono serikali ya mpito iliyo mpindua Muammar Gaddafi.
Taher Elmagrahi, alitangaza kuiunga mkono serikali ya mpito na kujiunga nayo baada ya serikali ya Muammar Gaddafi kung'olewa hivi karibuni na jeshi la wapinzani.
Simbarashe Mumbengegwi waziri wa mambo ya nchi za nje wa Zimbabwe alisema " Elmagrahi na wafanyakazi wote wa ubalozi wanatakiwa kuondoka nchini katika kipindi cha masaa 72."
Hata hivyo Taher Elmagrahi aliseme " mimi siyo mtu wa Muammar Gaddafi nipo kwa aajili ya Walibya na nawakilisha Walibya."
Serikali ya Zimbabwe na Libya zimekuwa na uhusiano wa karibu sana, hasa kati ya Muammar Gaddafi na rais Robert Mugabe.

1 comment:

Anonymous said...

Right away I am going away to do my breakfast, once having my breakfast coming yet again to read additional news.


my webpage :: valmorel