Sunday, September 25, 2011

Rekodi ya mbio za marathoni za Berlin ya vunjwa.

Rekodi ya mbio za marathoni za Berlini ya vunjwa.

Berlin, Ujerumani 15/09/2011. Mwana riadha Patrick Makau amevunja rekodi ya dunia ya mbio za marathoni iliyokuwa ikishikiliwa na mwanariadha Haile Gabreselassie wa Ethiopia.
Patrick alivunja rekodi hiyo kwa muda wa masaa 2 dakika tatu na sekunde 38.
Mwanariadha huyo aliwaongoza katika kipindi cha kumalizia mbio na huku Wakenya wenzake walishikiria nafasi ya pili na ya tatu katika mbio hizo.
Akiongea baada ya mbio hizo Partick alisema " sikujua kama siku kama ya leo inaweza kuwa kama ilivyo tokea nichofanya nilikuwa nimekuja kushindana na kushinda."
Haile Gabrselassie ambaye naye alishiriki mashindano hayo kwa kukimbia hadi kufikia km 35 na kujitoa.
Wanariadha wa Kenya wamekuwa wakiwika katika mbio na kuliletea taifa la Kenya sifa nyingi kila mwaka.
Dmitry Medvedev apendekeza Vladmir Puttin kugombea kiti cha urais wa Urusi.
Moscow, Urussi- 25/09/2011. Rais wa Urusi amemtangaza rasmi waziri mkuu wake Vladimir Puttin kuwa mgombea wa kiti cha urais katika uchaguzi unaotarajiwa kufanyika mwakani.
Dmitry Medvedev alisema " ninayo furaha kuwatangazia ya kuwa napendekeza waziri mkuu Vladimil Puttin kugombea kiti cha urais katika uchaguzi unaokuja na sina wasiwasi wowote wa kuwa na mashaka kwani naamini ni mtu mwenye uwezo mkubwa wa kuongoza nchi yetu."
Baada ya kutangazwa kwake kugombea kiti cha urais, Vladimir Puttin alisema " nipo tayari kuongoza Urussi kwa kusaidiana na wanzangu na Dmitry Medvedev atakuwa waziri mkuu kama tukishinda uchaguzi."
Huku wakishangiliwa na wanachama wa chama tawala cha United Russia walioudhuria katika mkutano mkuu wa chama hicho uliyo fanyika jijini Moscow, viongozi hao walionyesha ukaribu wa zaidi hata wakati walipokuwa wakiingia katika ukumbi wa mkutano.
Ufalme wa Saud Arabia watoa ruhusa kwa wanawake kupiga kura.
Riadh, Saudi Arabia - 25/09/2011. Mfalme wa Saud Arabia ametoa ruhusa kwa wanawake wote aliopo nchini Saudi Arabia kugombea nafasi za uongozi katika ngazi za manispaa na ruhusa ya kupiga kura.
Mfalme Abdullah bin Abdulaziz al Saud alisema " hatutaki kuwatenga wanawake kwani wao ni sehemu ya jamii baada ya makubaliano kufikiwa na kamati ya uongozi ya kifalme."
Kufuatia maelezo ya ya Mfalme, wanawake wote raia wa Saudi Arabia wataruhusiwa kikamilifu kushiriki katika uchaguzi wa manispaa utakao fanyika mwakani.
Inaaminika zaidi ya wanawake 5,000 huenda wakashiriki katika harakati za kupiga kura na kugombea uongozi katika manispaa 285 zilizopo nchini humo.

No comments: