Thursday, September 22, 2011

Mauaji ya kutisha yatokea Burundi.

Mauaji ya kutisha yatoke Burundi.
Bujumbura, Burundi - 22/09/2011.Kamishna mwenyekiti wa umoja wa Afrika amelaani matukio ya mauaji ya watu 40 yaliyo tokea hivi karibuni nchini Burundi.
Dr Jean Ping alisema " kitendo kilicho fanyika ni cha kinyama na umoja wa Afrika utaendelea katika jitihada za kuunga mkono kuwepo kwa amani nchini Burundi."
Mauaji hayo ambayo yametokea maeneo ya Gatumba, yameleta mshituko mkubwa kwa wanchi wa Burundi, na kutaka serikali ifanye kila njia kuwakamata wale wote walio husika, ilikuweza kuurudisha imani kwa wanachi.
Wanawake wawili wahukumiwa kwa kuvaa baibui nchini Ufaransa.
Paris
Ufaransa - 22/09/2011. Mahakama jijini Paris imewatoza faini wanawake wawili kwa kosa la kuvaa baibui zinazo funika hadi uso.
Wanawake hao walitozwa jumla ya euro 200 na mahakama hiyo baada ya kukutwa na hatia ya kuvunja sheria inayo zuia mavazi hayo.
Hata hivyo faini hiyo ililipwa na mfanya biashara mmoja na kusema " nadhani uhuru wa mtu ni muhimu sana, na sikubaliani na sheria iliyo wekwa kwani inakwenda kinyume na katiba ya Ulaya, nna wanawake lazima wawe huru hata wanapo tembea."
Faini hiyo imekuwa ya kwanza tangu kupitishwa kwa sheria ya kukutaza mavazi ya baibui inayo funika hadi usi, jambo baadhi ya wananchi wa Ufaransa wanapingana lao.

1 comment:

raypaptz2000 said...

Kama taratibu za kuvaa katika nchi ya Ufaransa na nchi zingine za ulaya ni marufuku kuvaa hijabu basi nao waarabu wapitishe sheria ya mtu kuvaa nguo fupi ua kaptura wafungwe tuone nao na mikaptura yao wataendaje huko arabuni