Friday, September 23, 2011

Wapalestina wakabidhi ombi la kutaka kutambulika kama taifa kwa Ban Ki-moon.

Wapalestina wakabidhi ombi lao la kutaka kutambulika kama taifa kwa Ban Ki-moon.

New York, Marekani - 23/09/2011. Rais wa Wapalestina amehutubia mkuutano mkuu wa umoja wa mataifa na kudai Palestina itambulike kama nchi huru pia kukabidhi maombi hayo kwa katibu mkuu wa umoja wa mataifa Ban Ki-moon.
Mahmoud Abbas akihutubia alisema " tunaweza kaa na kuzungumza na Izrael kwa kufuatia mkataba wa makubaliano ya mpaka mwaka 1967,na kusimamisha ujenzi wote unaoendelea katika maeneo ya Wapalestina, kwani mazungumzo ya hapo awali yalikwama kutokana na Izrael kutokuwa na nia ya kufanya mazungumzo mwaka jana Septemba."
Rais huyo wa Wapalestina alimaliza hotuba yake hiyo kwa kushangiliwa na viongozi wakuu wa nchini na wajumbe wote waliokuwemo ndani ya jumba la mkutano.
Hata hivyo waziri mkuu wa Izrael Binyamin Netanyahu ambaye naye alihutubia katika mkutano huo alisema " siwezi kuleta amani peke yangu, nasiwezi bila wewe Abbas, kwani sisi wote ni watoto wa Abraham."
"Inabidi Waizrael wafanye uamuzi busara kwa kukubali ya matakwa ya Wapalestina na vilevile Wapalestina lazima wafanye uamuzi busara kwa kukubaliana na matakwa ya Waizrael." aliongezea Netanyahu.
Hata hivyo ombi la Waplestina litachukuwa muda kabla ya kufikiwa muafaka wake na kikao cha kamati ya usalama ya umoja wa mataifa.
Rais wa Iran azilaumu nchi za Magharibi.
New York, Marekani - 23/09/2011. Rais wa Iran amezilaumu nchi za magharibi kwa kutumia uwezo walionao kuvuruga amani na kusababisha myumbo wa uchumi duniani.
Mahmoud Ahmadinejad akihutubia katika mkutano mkuu wa umoja wa mataifa alisema " nguvu za kijeshi zimekuwa zikitumika na mataifa ya magharibi pasivyo halali"
Pia mashabulizi ya Sept 11 ni ya kimiujiza, ingefaa Osama bin Laden akamatwe ili afikishwe kwenye sheria na tungejua ukweli, kwani kitendo cha kumwua hakikuwa na mantiki yoyote " alisisitiza rais Ahmedinejad.
Hata hivyo wakati akihutubia, viongozi wa nchi za magharibi walitoka nje ya jumba la mkutano baada ya rais huyo wa Iran kuanza kuzishambulia nchi hizo na hasa nchi ya Izrael.
Zambia yapata rais wa tano tangu kupata uhuru.
Lusaka, Zambia -23/09/2011. Kiongozi wa chama cha upinzani nchini Zambia ameshinda kiti cha urais kwa kumpita mpinzani wake wa chama tawala cha MMD- Movement for Mult-party democracy.
Michael Sata ambaye aligombea kiti cha urais kupitia chama cha Patriotic Front alishinda kwa kupata asilimia 43 za kura zidi ya mpinzani wake Rupia Banda.
Akihutubia baada ya matokeo ya uchaguzi, rais mpya wa Zambi Michael Sata alisema " wananchi wa Zambia wamesema na lazima tuwasikilize na huu ni wakati wa kuwa pamoja katika kuijenga nchi, kwani sisi vizazi vya zamani lazima tuwape mwelekeo mzuri wa kujenga nchi hawa vijana wa vizazi vipya."
"Na haidi kiweka Zambia kwanza na kupambana na rushwa" alisema rais mpya wa Zambia Michael Sata.
Rais Michael Sata ni rais wa tano tangu Zambia kupata uhuru mwaka 1964

No comments: