Sunday, September 4, 2011

Wanariadha wa Kenya hawana mpinzani duniani.

Muammar Gaddafi alishirikiana CIA na MI6.
Tripol, Libya - 04/09/2011.Jumuiya ya kutete haki za binadamu zimeilaumu serikali ya Uingereza na Marekani kwa kushirikiana na serikali ya Muammar Gaddafi wakati alipo kuwa madarakani.
Habari zilipo patikana zinasema "serikali ya Muammar Gaddafi ilikuwa ikishirikiana na makachelo wa CIA na MI6 na hata kuweza kutoa habari za wapinzani wa Gaddafi ambao walikuwa wanashukiwa ni magaidi, jambo ambalo lilifanya Walibya waliokuwa wamekimbia utawala wa Muammara Gaddafi kurudishwa nchini humo kwa mahojiano ili kuweza kujua kama ni magaidi au wanashirikiana na Al Qaeda."
Makaratasi zenye ripoti hizo yalikutwa kwenye ofisi inayo sadikiwa ilikuwa ya aliyekuwa mkuu wa usalama Moussa Koussa, ambaye kwa sasa anaishi nchini Katar baada ya kutoraka kwa kupitia Uingereza.
Muammar Gaddafi alikuwa mmoja wa viongozi walioshirikiana na Uingereza na Marekani katika kupambana na ugaidi na hasa kundi la Al Qaeda tangu vita rasmi vilipo tangazwa zidi ya ugaidi duniani baada ya mashambulizi ya 11/Sept 2001.
Angola ya kumbwa na vuguvugu la mabadiliko ya kisiasa.
Luanda, Angola -04/09/2011. Watu zaidi ya 23 wamekamatwa jijini Luanda baada ya kufanya maandamano ya kutaka rais Jose Eduardo dos Santos ajiudhulu.
Maandamano hayo yalianzia kwenye viwanja vya uhuru ili kuelekea kwenye ofisi za rais, kwa kuwa na lengo la kudai rais Jose Eduardo dos Santos aachie madarakani na watu walio kamatwa na kuwekwa kizuizini waachiwe huru.
Kwa mujibu wa habari zilizo patikana kutoka shirika la habari la Ureno Lusa zinasema " kuna baadhi ya watu wameumia vibaya wakiwemo waandishi wa habari, baada ya polisi na mafisa usalama kutumia nguvu katika kuzuia maandamano hayo."
Maandamano hayo yanakuja baada ya wanchi na viongozi wa upinzani nchini humo kudai ya kuwa "serikali ya Angola imekuwa haifanyi jitihada za kupambana na rushwa."
Angola inawananchi wapatao 16 milllion ambao wengi wao wanaisha chini ya dola 2 kwa siku.
Wanariadha wa Kenya hawana mpinzani duniani.
Daegu, Korea ya Kusini - 04/09/2011. Timu ya wanariadha wa Kenya wameweza tena kwa mara nyingine kuwanyanyu wananchi wa Afrika ya Mashariki na kuipatia sifa kubwa Kenya kwa kuweza kushinda medali za dhahabu kwa wingi kwenye mashindano ya riadha ya dunia nchini Korea.
Wanariadha hao wa Kenya wameweza kunyakua medali saba, na kukamlisha idadi ya medali kumi na sita katika mashindando hayo ambayo yanaisha wiki hii.
Vivian Cheruiyot ambaye ni mmoja ya washindi wa medali zilozo ipa sifa Kenya na Afrika ya Mashariki alisema " ushindi wetu unatokana na ushirikiano mkubwa tulionao wanariadha wa Kenya."
Wanariadha wa Kenya wamekuwa wanashinda mashindano mengi ya kimataifa na kuipatia Kenya sifa kila mwaka wanapo shiriki mashindano ya riadha popote duniani.
Dominique Strauss-Kahn arudi nyumbani akiwa huru.
Paris, Ufaransa - 04/08/2011. Aliyekuwa mkurugenzi mkuu wa shirika la fedha (IFM) duniani
amewasili nchini Ufaransa baada ya kesi ya ubakaji zidi yake kufutwa hivi karibuni.
Dominique Strauss Kahn, aliwasili jijini Paris na kupokelewa na baadhi ya watu waliokuja kumlaki na hakuweza kuongea na waandishi wa habari.
Hata hivyo Strauss Kahn anakabiliwa na kesi nyingine iliyo funguliwa zidi yake na na mwandishi mmoja kwa madai "alitaka kumbaka miaka ya nyuma."
Kwa mujibu wa wafuatiliaji wa mambo ya kisiasa wa Ufaransa wanasema "kesi hizi zimemwalibia kwa kiasi kikubwa Dominique Strauss Kahn katika kampeni yake ya kutaka gombea urais nchini Ufaransa na itabidi atumie busara ili kuweza kurudisha matumaini yake ya kutaka ugombea urais."
Uchaguzi wa urais nchini Ufaransa unatarajiwa kufanyika hapo mwakani.
Muuguzi akanusha uvumi kuhusu Muammar Muammar Gaddafi.
Mogolnoye
,Ukraine -04/09/11. Mmoja wa wauguzi wa Muammara Gaddafi amekanusha madai yaliyokuwa yameenea ya kuwa kiongozi huyo Libya alikuwa na uhuusiano wa kimapenzi na baadhi ya wauguzi na walinzi wake wa kike.
Oksana Balinskaya muuguzi aliyekuwa wa Muammar Gaddafi alisema " nashangaa kusikia uvumi huo, kwani hakuna hata siku moja kati yetu alikuwa anamtibu (Dady) Muammar Gaddafi peke yake, muda wote tulikuwa tumezungukwa na watu, kama si walinzi basi watu wa falimia yake."
"Tulikuwa tuna mwita dady, kwani alivyo kuwa na ukarimu, muda wote alituuliza kama tuna shida au tunataka kitu tuseme, hivyo siwezi kusema vibaya juu yake, bila yeye nisingeweza kua hapa nilipo kimaisha nitasikitika kama akiuwawa au kukamatwa."
Oksana Balinskaya ni mmoja ya wauguzi ambao walikuwa nchini Libya ili kufanya kazi ya uuguzi wakati wa utawala wa Muammar Gaddafi ambaye ameng'olewa madarakani hivi karibinu.

No comments: