Monday, September 5, 2011

Njaa yazidi kutishia maisha ya Wasomalia.

Izrael yakataa kuomba msamaha kwa Uturuki.
Tel Aviv, Izrael - 05/09/2011. Waziri mkuu wa Izrael imekataa kuomba msamaha kwa serikali ya Uturuki
Binyamin Netanyahu alisema " hatuna haja ya kuomba msamaha, ingawaje tunasikitika kitendo cha watu kupoteza maisha, kwani jeshi letu lilibidi lijilinde kufuatia mashambulizi yaliyofanywa na watu waliokuwemo kwenye meli hiyo, natumaini tukaweza kumaliza swala hili kimsingi, kwani Izrael haijawahi kutaka kukosana na Uturuki."
Maelezo hayo wa waziri mkuu wa Izrael yamefuatia ripoti iliyo tolewa na umoja wa mataifa kuhusu chanzo cha vurugu zilizo tokea kwenye meli iliyo kuwa imewabeba wana harakati wanao unga mkono Wapalestina, baada ya jeshi la Izrael kuivamia meli hiyo wakati ikielekea Gaza mwaka 2010 Mei.
Kutokana na tukio hilo serikali za Uturuki na Izrael zimefunga uhusiano wa kibalozi kati ya nchi hizo.
Wapinaji wa NTC nchini Libya wangoja amri baada ya mazungumzo kushindikana.
Bani Walid,Libya -05/05/2011. Mazungumzo kati ya jeshi linalo muunga mkono Muammar Gaddafi na jeshi serikali ya mpito yamekwama baada ya kutofikia makubaliano.
Mazungumzo hayo ambayo yalikwama baada ya wapiganaji wanao muunga mkono Muammar Gaddafi kukataa kusalimu amri.
Mkuu wa majadiliano wa serikali ya mmpito Abdallah Kanshil alisema " tumeshindwa kufukia makubaliano na sasa uamuzi tume waachia viongozi wetu waamue la kufanya."
Kuvunjika kwa mazungumzo hayo huenda kufanya jeshi la serikali ya mmpito lilipo km 10 kuanza mashambulizi katika mji wa Bani Walid, jambo ambalo linashukiwa litaketa maafa makubwa.
Kesi zidi ya Jacques Chirac kuendelea.
Paris, Ufaransa - 05/09/2011. Mahakama nchi Ufaransa imeamuru kesi zidi ya rais Jacques Chirac iendelee ijapokuwa hatakuwepo mahakamani kutokana na matatizo ya kiafya.
Chirac 78 anakabilwa na kesi ya kutumia pesa za umma vibaya wakati akiwa meya wa jiji la Paris.
Jaji Dominique Pauthe alitoa amri hiyo kwa kusema " hakuna haja ya kuwepo kwa mshitakiwa na kesi inaweza kuendelea."
Jacques Chirac wakati wa utawala wake alipinga kitendo cha kuvamiwa kwa nchi ya Irak na kama akikutwa na hatia anaweza kufungwa kifungo cha hadi miaka 10 na faini ya euro 150,000.
Njaa yazidi kutishia maisha ya Wasomalia.
Mogadishu, Somalia -05/09/2011. Mamia ya wananchi wa Somalia wamepoteza maisha kutokana na njaa na ukame uliyoikumba nchi hiyo.
Habari kutoka shirika la umoja wa mataifa linalo shughulikia lishe kwa ajili ya Somali zinasema " robotatu ya nchi ya Somalia imekumbwa na ukame na kusababisha njaa ambao imepelekea watu zaidi kupoteza maisha wengi wao wakiwa watoto wadogo."
Kufuatia hali hiyo, kitengo cha kutathmini hali ya lishe nchini Somalia kimeomba mashirika ya kimataifa kutoa mchango wao, au huenda zaidi ya watu 400,000 wakapoteza maisha kwa kipindi cha miezi michache kutoka sasa.
Somalia ni nchi moja wapo ya zile nchi zilizo kumbwa na ukame katika ukanda wa Afrika ya Mashariki.
Kesi zidi ya mpinzani wa serikali ya Rwanda kuendelea.
Kigali Rwanda -05/09/2011. Jaji wa mahakama nchini Rwanda ameamuru kesi zidi ya kiongozi wa upinzani Victoire Ingabire iendelee.
Jaji Alice Rilisa aliamuru kesi iendelee, baada ya mwanasheria kwa upande wa mshitakiwa kupinga ombi la upande wa mwanasheria wa serikali la kutaka kuongezewa muda ili kukusanya ushahidi zaidi.
Iain Edward wakili wa upande wa mshitakiwa aliomba mahakama kuruhusu kuendelea kwa kesi kwa kusema " mwendesha mashitaka wa serikali alisema wapo tayari kuuendelea na kesi na wanaushahidi wa kutosha tayari kuanza kusikilizwa kwa kesi hiyo inakuwaje wanataka waongezewe muda zaidi?"
Victoire Ingabire ambaye ni kiongozi wa chama cha upinzani nchini Rwanda cha Unified Democratic Force anashitakiwa kwa kwa kueneza chuki za kikabila, kukana kutokea mauaji ya kimbari nchini humo na kula njama za kutaka kununua siraha kwa ajili ya kutaka kuleta machafuko nchini Rwanda, na kama akikutwa na hatia huenda akafungwa kifungo cha maisha.

No comments: