Friday, September 2, 2011

Umoja wa Ulaya kuibana zaidi serikali ya Syria.

Polisi wazuia maandamano ya kimageuzi nchini Uganda.

Kampala, Uganda-02/09/2011. Serikali ya Uganda imepiga marufuko maandamano yaliyo kuwa yamepangwa ili kuungamkono mageuzi ya kisiasa yanayo endelea katika bara la Waarabu.
Uamuzi huo wa serikali umekuja baada ya habari kupatikana ya kuwa "uenda maandamano hayo yakaleta chuki kati ya jamii na kuwa mwazo wa mvurugo wa amani ndani ya nchi."
Hata hivyo msemaji wa polisi Vicent Sekate alisema " maandamano hayo yamezuiliwa kutokana na kukusa sehemu ya kuyafanyia."
Hivi karibuni rais Yoweri Museni alisema " mgeuzi yanayo tokea Kaskazini mwa Afrika yanaweza leta athari kubwa kwa bara la Afrika na kusababisha mvutano wa madaraka na kijeshi."
Serikali ya Uganda imekuwa na wakati mgumu kisiasa kutokana na joto lililomo nchini humo la kutaka serikali ya rais Yoweri Museni kufanya mabadiliko ya kiuchumi.
Umoja wa Ulaya kuibana zaidi serikali ya Syria.
Brussels, Ubeligiji -02/09/2011. Umoja wa nchi wanachama wa jumuiya ya Ulaya zimeamua kwa pamoja kuiwekea vikwazo serikali ya Syria kutokana na kukiuka haki za binadamu.
Uamuzi huo umekubalika na viongozi wa jumuia ya Ulaya ili kuibana serikali ya Syria chini ya rais Bashar al-Assad ambayop inapambana na wapinzani wanaotaka mageuzi ya kisiasa nchi humo.
Waziri mkuu wa Uingereza David Cameron alisema " tunatakiwa kuiwekea vikwazo serikali ya Syria kwani vitendo vinavyo fanywa na serikali hiyo havikubaliki."
Vikwazo hivyo ambavyo ni kuzuia ununuzi na uuzwaji wa mafuta ya Syria na kuongeza vikwazo vya usafiri kwa wale wote wanaohusika katika serikalia ya rais Assad vimesha tayarishwa na vinasubiri kujadiliwa wakati wa mkutano wa mawaziri wa mambo ya nchi za nje wa nchi hizo na baadaye kupitishwa.
Machafuko nchini Syria yamezidi kuongezeka, kufuatia mageuzi ya kisiasa yaliyo likumba bara la Waarabu hivi karibu.
Uturuki yapunguza uhusiano na Izrael.
Ankara, Uturuki -02/09/2011. Serikali ya Uturuki imeamua kupunguza uhusiano uliopo kati yake na serikali ya Izrael.
Waziri mkuu wa Uturuki Ahmet Davutoglu aliyaongea hayo muda mfupi kabla ya katibu mkuu wa umoja wa mataifa Ban Ki-moon kukabidhiwa ripoti kuhusu tukio la jeshi la Izrael na wanaharakati waliokuwa wanelekea maeneo ya Gaza ili kupeleka misaada ya kiutu.
Serikali ya Uturuki imekuwa ikiitaka serikali ya Izrael kuomba msamaha baada ya raia wa Uturuki kuuwawa katika boti zilizokuwa zunaelekea Gaza hapo siku za nyuma.
Pia Uturuki imefunga ofisi zake za kibalozi nchini Izrael na kumtaka balozi wa Izrael nchini humo aondoke mara moja na kusimamisha ushirikiano wa kijeshi uliopo kati ya nchi hizi mbili.
Mvutano kati ya serikali ya Uturuki na Izrael ulizidi kuwa wa wasiwasi baada ya jeshi la Izraeli kufanya mashambulizi kwenye maeno ya Gaza miaka miwili iliyo pita na watu wengi kupoteza maisha na malinyingi kuharibiwa.

No comments: