Thursday, September 8, 2011

ZANU-PF yakansha madi ya kuwa Robert Mugabe anasatani.

ZANU-PF yakanusha madai ya kuwa rais Robert Mugabe anasatani.
Harare, Zimbabwe - 08/09/2011.Msemaji wa chama tawala ZANU-PF nchini Zimbabwe amekanusha habari za uvumi ya kuwa rais wa nchi hiyo anasaratani ya muda mrefu.
Habari kutoka kwenye chama hicho zinasema " habari zilizo tolewa na Wikileaks ya kuwa gavana wa benki kuu ya Zimbabwe aliongea faragha na balozi wa Marekani Christopher Dell mwaka 2006 ya kuwa rais Robert Mugabe anasumbuliwa na saratani ambayo imesambaa karibu mwili mzima siyo kweli."
"Kama ilikuwa mwaka 2006 ndiyo walifanya mazungumzo hayo mbona mpaka leo yupo mzima na hakuna hata siku alionekana yupo dhaifu." habari kutoka ZANU-PF zilisema.
Ukanushi wa habari hizo , umekuja baada ya mtandao wa Wikileaks kutoa habari ya kuwa rais Robert Mugabe anasadikiwa kuwa na ugonjwa wa saratani.
Kiongozi wa serikali ya mpito ya Libya awasili nchini kwa mara ya kwanza.
Libya, Libya - 08/09/2011. Kiongozi wa serikali ya mpito iliyo leta mapinduzi ya kijeshi nchini Libya amewasili nchini Libya kwa mara ya kwanza tangu kuanza mapinduzi hayo.
Mohmoud Jibril aliwasili nchini Libya ili kuangalia maendeleo na kuzungumza na wapiganaji waliongoza katika kuing`oa serikali ya Muammar Gaddafi.
Katika mikutano tofauti aliyo udhulia na kuhutubia, Mohmoud Jibril alisema "kazi ya kuikomboa Libya bado na haitakuwa vizuri tukiaanza kulumbana kisiasa, kwani mbele yetu bado kuna kazi kubwa ya kufanya ili kuijenga upya Libya."
Wakati huo huo, wapiganaji wanaomuunga mkono Muammar Gaddafi walifanya mashambuli zidi ya jeshi la wapinzani karibu na maeneo wanayo shikilia, baada ya kiongozi huo kutangaza yakuwa yupo nchini Libya na akatoa wito waendelee kupambana na wapinzani.
Vita kati ya wapiganaji wa serikali ya mpito na wale wanaomuunga mkono Muammar Gaddafi yamekuwa yakiiendelea kwa muda wa miezi sita tangu harakati za mapinduzi kuanza nchini humo.

No comments: