Tuesday, January 31, 2012

Marekani yadai utawala wa rais Bashar al Assad wa Sryia utaanguka muda si mrefu.

Senegal yaingia katika mtego wa demokrasi na vurugu katika bara la Afrika.

Dakar, Senegal-31/01/2012. Maalfu ya wananchi nchini Senegal , wakiongozwaa na viongozi wa vyama vyaupinzni wana endelea kuandamana ili kupinga uamuzi wa mahakama kuu kumruhusu rais wa sasa Abdoulaye Wade kugombea kiti cha urais kwa mara ya tatu.
Maanamno yao ambayo yameaanza siku hivi karibuni yamesha poteza maisha ya watu wawili  baada ya kupigwa risasi wakati wa maandamano ambayo yalizuiliwa na polisi na kusababisha vurugu.
Uongozi wa chama cha upinzani June 23 Movement - M23 umewataka wananchi "kuandamana bila kufanya vurugu."
Vurugu za kisiasa nchini Senegal zimekuja baada ya mahakama kuu nchini humo kutoa ruhusa kwa rais Abdoulaye Wade kugombea kiti cha urais na kuwaazuia baadhi yawagombea akiwemo Yousuf Ndour kwa kutotimiza masharti ya uchaguzi.

Marekani yadai utawala wa rais Bashar al Assad wa Syria utaanguka muda si mrefu.

Washington, Marekani - 31/01/2012. Serikali ya Marekani imedai ya kuwa serikali ya rais Bashar al Assad inakaribia kuanguka.
Matamshi hayo ya Marekani yamekuja wakati jumuiya ya nchi za Kiarabu zimewakilisha  muswada ili se rais Bashar al-Assad aachie  madaraka ili kuwezesha kuundwa kwa serikali ya mpito itakayo andaa uchaguzi wa halari nchini Syria.
Msemaji wa Ikilu ya Marekani Jim Carney alisema " kuanguka kwa serikali ya Bashar al- Assad kupo njiani kwani haina tena utawala katika nchi nzima ya Syria."
Hata hivyo serikali ya Urussi imedai " mswada huo wa nchi za Kiarabu inafungua njia ya vita vya wenyewe kwa wenyewe."
Syria imekumbwa na mvurugo wa kisiasa tangu kuibuka kwa mwamko wa kisiasa katika nchi za Kiarabu ambao ulianzia nchi Tunisia.


Makamu wa rais wa Irak aonya kurudi kwa vita vya wenyewe kwa wenyewe nchini Irak.


Irbil, Irak - 31/01/2012. Makamu wa rais wa Irak ambaye yupo ukimbizini katika jimbo la Kikurdishi ameonya yakuwa Irak inawezza kurudi katika vita vya wenyewe kwa wenyewe.
Makamu wa rais Tariq al-Hashimi alisema " Hali iliyopo nchini Irak kwa sasa inatisha na inaelekea kukaribisha vita vya wenyewe kwa wanyewe, kwa Waziri Mkuu Nuri al-Maliki anaielekeza nchi yangu kwenye hali ya kuwepo vita kati yetu wenyewe kwa wenyewe."
"Nashangaa kusikia ya kuwa Irak ni bora kwa sasa, na Marekani inawezaje kujisifia kutokana na hali iliyopo nchini Irak? Wakati hali bado ni tete kila sehemu, Irak kutokuwa na amani kutaathiri maslahi ya Marekani."
Makamu wa rais Tariq al-Hashimi yupo ukimbizini katika jimbo la Wakurdishi, baada ya kushutumiwa kuhusika katika njama ya kutaka kuleta machafuko ndani ya serikali.


Nchi wanachama wa muungano wa Ulaya wakubaliana kudhibiti sarafu ya Euro.

Brussels, Belgium - 31/01/2012.  Nchi za muungao wa jumuiya ya Ulaya zimekubaliana kwa pamoja kudhibiti matumizi ya fedha kwa nchi wanachama katika kikao ch wakuu wa nchi hizo walipo kutana nchi Belgium.
Katika mkutano huo viongozi hao wa nchi 25 walikubli na kutia sahii mkataba wa kudhibiti, ili kuepusha hali iliyoo tokea hivi karibuni ya kuyumba kwa mfumo wa kifedha katika nchi za muungano huo.
Rais wa muungano wa nchi hizo za Ulaya Herman Van Rompuy alisema " nivizuri tumeweza kutimiza na kukubaliana kwa pamoja na hi itasaidia kuimarisha sarafu ya euro katika soko la kimataifa."
katika mkataba huo nchi mbili Uingereza na Jamuhuri ya Chezch zimekataa kusaini mkataba huo kutokana na sababu za ambazo nchi hizo zinasimamia kwa manufaa ya nchi zao.




No comments: