Sunday, May 27, 2012

Mshukiwa wa kusambaza siri za Kanisa akamatwa.

Matamshi ya Christine Lagard yawasumbua wa Wagiriki.


London, Uingereza -27/05/2012. Mkuu wa shirika la fedha duniani International Monetary Fund (IMF) Christine Lagard ameshutumiwa na kulaumiwa na wanasiasa wa Ugiriki kutokana na kauli aliyo toa kuhusu nchi hiyo katika maswala ulipaji wa kodi za mapato na kutimiza masharti yaliyowekwa na nchi wanachama wa jumuiya ya Ulaya.
Kiongozi wa chama cha Kisoshaliti Eangelos Venizolos alisema  "matamshi ya mkuu huyo kuhusu Ugiriki ni kuwatukana Wagiri.
"Wagiriki tunalipa kodi na hakuna raia wa Ugiriki asiyelipa kodi."
Shutuma hizo zilikuja baada ya Christine Lagard kuseme " mimi ninawasiwasi na Wanchi waliopo  Kusini mwa Jangwa la Sahara barani Afrika kwani wao wanaitaji msaada kuliko wananchi wa Ugiriki"
Matamshi hayo ya mkuu huyo wa shirika hilo la fedha duniani IMF yamekuja  wakati wananchi wa Ugiriki wana wakati mgumu wa kiuchumi huku wakiwa wanajiaandaa na uchaguzi wa serikali itayo takiwa kutimiza masharti ya jumuiya  ya nchi za Ulaya katika kufanya marekebisho ya kiuchumi.


Mshukiwa wa kusambaza siri za Kanisa Katoliki akamatwa.

Vatikan, Vatikan City - 27/05/2012. Ofisi ya makao makuu ya Kanisa Katoliki imetangaza ya kuwa aliyekuwa msaidizi wa Papa Benedikt XVI amekamatwa.
Habari kutoka ofisi ya Kanisa hilo zilisema £Paolo Gabriele 46, alikamatwa mapema wiki hii siku ya Jumatano, baada ya mafaili yenye maelezo ya ambayo yanayo husu Papa Benedikt VXI na shughuli nyingine za kikanisa kukutwa nyumbani kwake."
Mtuhumiwa huyo ambaye alishawahi kufanya kazi katika ofisi za Papa Benedikt XVI mwaka 2006, na wakati huo alikuwa na uwezo wa kuona shughuli zote alizo kuwa anafanya Papa.
Kukamatwa huko kwa Paolo kumekuja baada ya habari za siri za kiofisi za Kanisa Katoliki Vatikani kusaambaa katika vyombo vya habari hivi karibuni.

Nchi za Ulaya Magharibi za agizwa kuondoa vikwazo zidi ya Zimbabwe. 

Harare, Zimbabwe - 27/05/2012. Mkuu wa  maswala ya haki za binadamu  wa umoja wa Mataifa amezitaka nchi za jumuiya ya Ulaya Magharibi, kuondoa vikwazo vilivyo wekwa zidi ya Zimbabwe.
Mkuu huyo Navi Pillay alisema hayo wakati akiwa ziarani nchini Zimbabwe na kudai " vikwazo vilivyo wekwa vinazidi kuwaumiza watu masikini na vinafanya jamii kubwa ya Wazimbwe kushindwa kuimarisha miradi mbalimbali na serkali  inakuwa na wakati mgumu  katika  ajira na kuinua maisha ya watu wenye kuishi maisha ya hali chini."
Zimbabwe iliwekewa vikwazo na nchi za Ulaya Magharibi mwaka 2008, kufuatia matokeo ya uchaguzi wa urais kwa madai ya kuwa  wakati wa kampeni za uchaguzi, wadau na wale wanao muunga mkono rais Robert Mugabe walishiriki katika ukiukwaji wa haki za binadamu.

Viongozi wa makundi ya Kiislaam waungana nchini Mali na kuunda serikali yao.

Azawad, Mali - 27/05/2012. Makundi mawili makubwa ambayo yanapingana na serikali kuu ya  Mali yametangaza kuungana na kuunda serikali ya Kiislam nchini Mali.
Makundi hayo ya kabila la Tuareg la National Movement for the Liberation of Azawad (NMLA) na Ansar Dine  yanayo shikilia  upande wa Mali ya Kaskazini, yalikubaliana kunda serikali hiyo ya Kiislam, baada ya viongozi wa makumndi hayo kukutana.
Kiongozi wa Tuareg  Alghabass Ag Intilla alisema " nimesaini mkataba na kukubali ushirikiano ili kuunda serikali itakayo ongozwa katika maadili ya Kiislam, na tutakuwa nchi huru ya Kiislam."
Makubaliano hayo ya viongozi wa makundi hayo mawili alikutana katika mji wa Gao na kusini mkataba hu.
Nchi ya Mali imekuwa na mvutano wa kisiasa na wakijamii kwa muda sasa tangu mapinduzi yalipo tikea nchi humu hivi karibuni.


No comments: