Friday, May 25, 2012

Rufaa ya Uhuru Kenyatta na wenzake yakataliwa na mahakama ya Uhollanzi. 

Rufaa ya Uhuru Kenyatta na wenzake yakataliwa na mahakama ya Uhollanzi. 


Nairobi, Kenya - 25/05/2012. Rufaa ya kesi inayo wakabili baadhi ya wanasiasa wa Kenya wanao shukiwa kuhusika na vurugu na mauaji yaliyo tokea nchini Kenya 2008 imekataliwa  na mahakama ya kimataifa inayo shughulikia utetezi wa haki za binadamu iliyopo nchi Uhollanzi.
Rufaa hiyo iliyo kuwa inatafuta uhalali wa mahakam hiyo ya Uhollanzi ilitupiliwa mbali, na kuweka uwezekano wa wanasiasa hao wa kutoka nchi Kenya kushitakiwa.
Watuhumiwa hao ni Uhuru Muigai Kenyatta, ambaye ametangaza kugombea kiti cha urais wakati wa uchaguzi 2013, William Rutto, Francis Muthauri, Joshua Arap Sang wana shutumiwa kwa kuhusika kwa njia moja au nyingine katika ghasi na vurugu zilizo sababisha maisha ya watu 1,200 kupoteza maisha na 600.000 kukosa makazi baada ya mali na makazi yako kuharibiwa kutokana na vurugu hizo.

Serikali yaombwa kuchunguza chanzo cha kifo cha Rashid Yakini.

Lagos, Nigeria - 25/05/2012. aliyekuwa  timu kaptaini wa timu ya taifa ya Nigeria ameiomba serikali ya Nigeria ifanya uchunguzi nini chanzo cha kifo cha aliyekuwa mchezaji maarufu na maili wa timu ya taifa wanchi hiyo Rashid Yakin 49.
Kamptan Segun Odegbami alisema " walimchukuwa kwa wiki tatu na wamemrudisha akiwa marehemu, lazima tujiulize alikuwa wapi katika kipindi chote hiki.
" Hakuna mtu yoyote anasema kwamba aliuwawa, na hakuna maelezo yoyote juu ya kifo chake, haiwezekani mchezaji maarufu wa bara la Afrika afariki bila hata uchunguzuzi wa kifo chake usifanyike?
"Naamini hata huko alipo kwenye kaburi lake, anaomba ukweli wa kifo chake ufahamike na tunacho weza kufanya ni kumwombe kwa  Mola aipumzishe roho yake pema pepono." alimalizia kaptain Segun Odegbami.
Marehemu Rashid Yakini alifariki Mei, 04/ 2012 na alikuwa  mfungaji namba tatu bora  katika mashindano ya kombe la Afrika kwa kufunga magoli 13 na mfungaji bora katika timu ya taifa ya Nigeria kwa miaka mingi kwa kufunga magoli 37. 

Mkutano wa Baghdad kuhusu Iran na nykilia waisha bila muaafaka. 


Baghdad, Irak - 25/05/2012. Mkutano wa uliyokuwa ukifanyika nchini Irak, ili kuzungumzia swala na nyuklia la nchi ya Iran limekwisha bila kufikia muafaka.
Waziri wa mambo ya nje ya nchi wanachama wa nchi za jumuiya ya Ulaya Catherine Ashton akiongea na waandishi wa habari mara baada ya kumalizika kwa mkutano huo alisema " mkutano umekwenda vizuri japo kuwa kuna baadhi ya maswala ambayo yanabidi yaafikiwe kutoka pande zote mbili."
Hata hivyo kwa mujibu  wa habari kutoka mwakilishi wa Iran katika mkutano huo Saeed Jalili alisema " swala la kuitaka Iran kusimamisha uzalishaji wa kinyuklia halita wezekana kwani Iran ina haki ya kufanya uzalisha huo kwa kufuata sheria za kimataifa na Iran inafanya uzalishaji wake kwa matumizi ya kisayansi na siyo kwa ajili ya kutengeneza siraha za kinyuklia."
Mkutano huo uliyofanyika nchi Irak, ulikuwa na mazumuni ya kuendeleza ushawishi wa kuitaka Iran isimamishe uzakishaji wake wa nyuklia, jambo ambalo Iran imekuwa ikilipinga kila kunapo kuwepo na mkutano wa kuzungumzia swala hilo.
Kikao kingine cha kujadili Iran na mradi wake wa kinyuklia unatarajiwa kufanyika nchi Urusi kama ilivyo pendekezwa kabla ya kuisha mkutano hu.

Rais wa Ufaransa afanya ziara ya ghafla nchi Afghanistan.

Kabul, Afghanistan - 25/05/2012. Rais wa Ufaransa amefanya ziara ya ghafla nchini Afghanistani na kufanya mazungumzo na wanajeshi wa jeshi la Ufaransa.
Rais Francois Hollandes alitangaza kwa kusema "  uamuzi wa kutoa jeshi letu nchi Afghanistan ni uamuzi wa nchi na washiriki wetu wa NATO wanalielewa hili bila utata na serikali ya Afghanistan inakubaliana na si bila kipingamizi chochote..
Na majeshi ya Ufaransa yatakuwa yamesha ondoka nchini Afghanistani ifikapo  mwisho wa mwaka huu."
Katika ziara hiyo rais Francois Hollandes amefanya mazungumzo na rais wa Afghanistan Hamid Karzai  ili kujadili ni kwa jinsi gani Ufaransa itasaidia katika kuijenga Afghanistan baada ya kuongoka kwa majeshi ya NATO mwaka 2014 kama ilivyo tangazwa wakati wa kikao cha viongozi wa NATO kilicho fanyika Marekani hivi karibuni.

Kifungo cha Muuguzi cha sababisha Marekani kusimamisha msaada wa fedha kwa Pakistani.


Washington, Marekani - 25/05/2012. Kamati ya bunge la Marekani linalo shughulikia maswala ya utoaji misaada imepiga kura na kuamua kusimamisha msaada wa kipesa inayo pelekwa Pakistan.
Uamuzi huo umekuja baada ya hukumu ya kwenda jela kwa miaka 33 aliyo pewa muuguzi  Shakil Afridi kwa kutoa habari za kisayansi DNA zilizo wezesha kuuwawa kwa kiongozi wa kundi la Al Qaeda Osama bin Laden mwezi Mei 2011.
Mbunge Richard Durbin alisema " Pakistan wanatakiwa watambue hatuna mzaha katika swala la ulinzi  nchi yetu na maslahi yetu, kwani ni kitu cha kushangaza kuona kuwa mtu aliye saidia katika kujua wapi alipo Osama bin Laden anaitwa msaliti."
Waziri wa mambo ya nje wa Marekani Hillary Clinton alisema " kitendo cha kumfunga  Muuguzi Shakil Afridi ni cha kinyume cha sheria na tuta zidisha hoja ya kutaka aachiwe huru, kwa Marekani hatuoni haki ya kufungwa kwake."
Marakani hua inatoa msaada wa kiasi cha $ dola za Kimarakani millioni 33, ikiwa ni moja ya fedha zinazo saidia kati shughuli mbalimbali za kujenga nchi ya Pakistani kiuchumi na kijamii.

No comments: